WAANDAAJI wa mbio za mwaka huu za Kumbukumbu za kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, marehemu Edward Sokoine, Sokoine
Memorial Mini Marathon 2014, wamezifanyia mbio hizo mabadiliko.

Akizungumza na LIBENEKE LA KASKAZINI mjini hapa, Mratibu wa mbio hizo,
Wilhelm Gidabuday, alisema mabadiliko hayo yanatokana na maombi
mbalimbali ya washiriki wa mbio hizo, kutokana na msimu huu kuwepo kwa
ratiba iliyobanana ya mashindano ya kitaifa na ya kimataifa.

"Tunaomba radhi kwa kufanya mabadiliko ya ghafla! Hiyo ni kutokana na
mashauriano kati yetu sisi waandaaji, Chama cha Riadha Mkoa na
wanariadha wenyewe, imeamuliwa kwamba siyo vizuri kuwakimbiza
wanariadha mbio ndefu mara mbili kwa wiki moja, sababu pia kutakuwa na
Tigo Ngorongoro Half Marathon Aprili 19, mwaka huu," alisema Gidabuday.

Aidha, Gidabuday alisema Kamati ya maandalizi ya mbio hizo inaishukuru
familia ya hayati Sokoine kwa kubariki mabadiliko hayo na kuongeza
kuwa, uamuzi huo mgumu umetokana na moyo wa kizalendo, kwani pamoja
na mbio za kitaifa kuna wanariadha washiriki ambao ratiba inaonesha
kuwa watakuwa na mbio za kimataifa nchini China mapema mwezi ujao.

"Familia ya Sokoine kwa moyo wa kizalendo zaidi, imeridhia ombi letu
na pia imekuwa wazo zuri kwa wanariadha wazoefu ambao wanafahamu
athari za kukimbia mbio ndefu mfululizo, pia wananchi wengi sasa
wataweza kushiriki kilomita 10," alisema Gidabuday.

Wakati huo huo, Gidabuday alisema taratibu zingine hadi sasa zipo kama
zilivyopangwa, ambako zoezi la kujisajili linaendelea Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid Karume kwa sh 2,000 tu.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia