Ticker

6/recent/ticker-posts

AJALI MBAYA YATOKEA SUYE JIJINI ARUSHA HIECE YAGONGANA USO KWA USO NA HILUX DOUBLE CABIN

10299515_698921726813920_5029549875143891989_n
Ajali mbaya imetokea  maeneo ya Suye katika barabara ya Mandela ambapo gari ya abiria Hice yenye namba za usajili T…. inayofanya safari zake kati ya Nduruma na katikati ya Jiji imegonganga us kwa uso na Toyota Hilux double Cabin mapema sana asubuhi majira ya saa moja na nusu. Kwa mujibu wa mashuhuda, inaelezwa kuwa dereva Daladala maarufu kama ‘Vifodi”amevunjika vunjika vibaya miguu yote miwili.
Chanzo cha ajali kinaelezwa kusababishwa ulevi wa dereva wa Hilux ambaye alikua amelewa kiasi cha kuyumbayumba barabarani. Dereva huyo baada ya kusababisha ajali alijaribu kukimbia  na watu kumzuia, akatoa bastola yake na kuleta kizaazaa kikubwa eneo la tukio ambapo barabara ilikuwa imefungika kwa mda hivyo kusababisha umati mkubwa wa watu kushuka kwenye magari na kulizunguka eneo hilo. Hata hivyo Polisi waliwahikufika na kumdhibiti na hali ya utulivu ikarejea.
10277168_698921906813902_4994584036942244635_n
1544607_698921680147258_5401702979124901094_n
1538897_698921770147249_6331144358783336375_n

Picha zote na Emmanuel Lukwaro

Post a Comment

0 Comments