Zaidi ya
wafugaji 300 wa kuku na mifugo mbalimbali na wafanyabishara wa maduka ya madawa ya kilimo na mifugo
wamepatiwa mafunzo ya utumiaji dawa mbalimbali za kutibu mifugo ya aina
mbalimbali na virutubisho mbalimbali vinavyotolewa na kampuni ya BYTRADE (T)
LTD ilikukwepa magonjwa ya mafuwa na aina nyingine za magonjwa na virutubisha
vya mifugo.
Akizungumza
katika semina ya kuwajengea uwezo wafugaji na wauza dawa za mifugo mkuu wa
idara ya wanyama wa kampuni ya Bytrade dkt Omary Magoma alisema kuwa aina
mbalimbali za mifugo zimekuwa zikisumbuliwa na maradhi mbalimbali na zinahitaji
dawa za kuyatibu maradhi yao ili kuweza kupata suluhu.
Magoma pia
akawataka wafugaji pindi wanapoona wanyama wao wana hali dhaifu kuacha kuwapa
dawa bila ya kugundua ugonjwa huku pia wakiendelea kuteketea na kuwashauri
kutumia bidhaa za kampuni hiyo kwani ndio suluhu ya matatizo ya magonjwa na
virutubisho ya wanyama na mimea.
“Kwa mfano
dawa hii ya GUT-O-CID ni dawa ya kudhibiti kwa ufanisi bacteria waenezao
magonjwa sumbufu kama salmonella,E.coli pia inadhibiti uzalishwaji wa gesi ya
ammonia inayosababishwa harufu kali bandani ambayo ni chazo cha mafua makali
kwa wanyama aina ya Kuku na Nguruwe”alisema dkt Magoma.
Dawa hiyo
ambayo huchanganywa kwenye chakula ukilinda chakula hicho dhidi ya maambukizi
ya bacteria na fangasi na pia huongeza ladha ya chakula akabainisha kuwa kwa
sasa wameingiza dawa aina kumi na moja sokoni na zinapatkana kwenye maduka
mbalimbali ya madawa ya mifugo humu
nchini.
Dkt Magoma
alizitaja baadhi ya dawa hizo kuwa ni suluhu ya maradhi yanayowaandama wanyama
wafugwao kwa mfano dawa hii ya Mult-Aminovet ina aina zote za vitamin na amino
acid pia madini kuweza kufidia mapungufu katika vyakula vya wanyama na
kuboresha kiwango cha utagaji na ubora wa mayai.
Pia
inaongeza matokeo bora kwa ng’ombe wa maziwa na hutumika kuondoa stress wakati
wa matibabu,chanjo,joto kali na usafirishaji kwa kuku huku pia akiitaja dawa
aina ya Enziver kuwa inaboresha uyeyushwaji na unyonywaji wa chakula mwilini
mwa wanyama na pia huraisisha ukuaji na ongezeko kubwa kwa kuku na nguruwe.
Huku akiwata
watanzania hususani wafugaji kuanza kutumia dawa za kampuni hiyo kwani ndiyo
suluhu ya kupata mifugo bora kwani dawa wanazouza zipo kwenye viwango vilivyo
bora.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia