Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Karatu
kimeeleza kufurahishwa kwake na mchango unaotolewa na Rais Jakaya
Kikwete katika kuchochea maendeleo bila upendeleo.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais, Ikulu, ilisema kuwa pongezi hizo zilitolewa jana mchana na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Titus Massey
wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini Karatu.
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na Chadema.
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na Chadema.
“Ni lazima tutoe shukurani kwako kwa sababu bila
wewe kuwa Rais wa Tanzania, sisi Karatu tusingepata jengo hili.
Pamoja na kwamba Halmashauri yetu ni Chadema bado umeamua kuchangia maendeleo ya wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo hili. Sisi hata robo ya fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” alisema Massey huku akishangiliwa na wananchi.

Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
limegharimu Sh1.412 bilioni na kati ya hizo, Serikali imetoa Sh1.394
bilioni na halmashauri imechangia Sh18 milioni.
Rais Kikwete alisema sera ya Serikali yake ni
kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali misimamo yao ya
kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa kila mtu
anataka maendeleo.