Nanyaro akisimulia mkasa halisi ulivyotokea
diwani wa LEVOLOSI Ephata Nanyaro akiwa anongelea tukio la yeye na kaimu meya kupigwa na mgambo wa jiji mbele ya waandishi wa habari
Wananchi ambao ni wafanya biashara wakimsikiliza meya wa jiji la Arusha mara baada ya kwenda ofisi kwake kulalamika juu ya manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa mgambo
Naibu mey a wa
halmashauri ya jiji la Arusha Prosper Msofe pamoja na diwani wa kata ya LEVOLOSI leo wamechezea kichapo kikali kilichowapelekea majeraha makali kutoka
kwa mgambo wa jiji
la Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari diwani wa
kata ya LEVOLOSI Ephata Nanyaro alisema
kuwa tukio hilo la wao kupigwa limetokea majira ya asubui katika depoti
ya manispaa ya jiji wakati
walipoamua kwenda katika eneo hilo mara baada ya kusikia wananchi ambao ni wamachinga wakiwemo wamama
wamekamatwa na kupelekwa katika depoti
hiyo ya manispaa ya jiji huku wakiwa
wanapigwa.
Diwani huyo alisema kuea naibu meya ameweza kupigwa sehemu mbalimbali
za mwili ikiweo miguuu ambapo kwa upande wake
yeye amueumizwa maeneo ya goti lake la kushoto ,mdomo pamoja na taya yake ya kushoto .
Aidha alibainisha kuwa wao kama madiwani
walipewa taarifa leo asubui kuwa kuna wananchi waliopo soko kuu wanapigwa
na askari mgambo wa jiji bila sababu yeyoyote
,huku akibainisha kuwa kisheria
mgambo ao walikuwa hawatendi
haki kwa jinsi waivyokuwa wanakamata
watu kwani walikuwa hawafati sheria ya nchi ,bali walikuwa wanaenda kinyume na
kanuni ya katiba ya nchi inasema usimpige mtu mara baada ya kumkamata bali umfikishe
katika mikono ya sheria ikiwemo polisi.
Akielezea maelezo ya awali naibu meya Prosper
Msofe alisema kuwa wao walipewa taarifa
kutoka kwa baadhi ya wafanya biahara wadogo wadogo kuwa wanakamatwa na
kupigwa pasipo sababu na vitu vyao vinachukuliwa hivyo ndipo
walipoamua kuwafata mgombo hao katika depoti yao na walivyofika yeye kama naibu
meya aliamua kuwaambia mgambo wale kwanini mnawapiga wananchi bure na sheria
hairuhusu kupiga mtu bali kumkamata
ndipo magambo wale waliwageuzia kibao na kuanza kuwapiga wao.
“sisi tulivyofika pale niliamua kuwauliza
vizuri mgambo wale kwanini mnawapiga wananchi mara baada ya kuwakamata badala
ya kuwachukulia sheria ya kuwapeleka polisi na sio kuwaweka huku depo basi mgambao wale ambao waikuwa zaidi ya 15 hawakuongea kitu bali walituambaia tu nyie
ndo mnajidai madiwani wenyeviere here na kuwamua kuanza kutushambulia”alisema msofe
Alisema kuwa kufuataia tatizo hilo la wanachi
kupigwa mara kwa mara mpaka sasa
wananchi zaidi ya watatu wameshavunjwa miguu huku wengine zaidi ya sitini
wameshapigwa favu na viboko na kati yao ,kunabaadhi yao ambao wame lazwa katika
hospitali ya mkoa ya mounti meru wakiwa wanatibiwa na halmashauri ambapo alibainisha kuwa pia wananchi hao
waliopigwa na kulazwa pindi watakapo pon a wanampango wa kuwafikisha mgambo hao
mahakamani kusiana na matukio hayo ya kuwapiga.
Akiongelea tukio hilo meya wa jiji la Arusha Gaudence
Lyimo alisema kuwa wao kama madiwani na
meya wa jiji amepokea kwa masikitiko makubwa
tukio hilo na alibainisha kuwa walichofanya mgambo hao wamekiuka sheria
bali alisema kuwa wamekaa kikao cha muda na wameamua kuwasimamisha kazi mgambo
wote kwa kitendo cha kuwazalilisha madiwani hao .
Alibainisha kuwa katika kipindi hicho ambacho madiwani hao
wamesimamishwa kazi wataunda kamati ya uchunguzi ambao itawashirikisha baadhi
ya madiwani pamoja na watendaji wa halimashauri
ili kujua na ni anamakosa kati ya madiwani na mgambo na iwapo itagundulika
ni mgambo basi watawachukuli hatua za kisheria.