LEMA AMJIBU RAIS KIKWETE ,HAPOHAPO AMTAKA OCD ARUSHA AACHE KAZI

Mkuu wa Polisi wilayani ya Arusha mjini (OCD), Gires Muroto,MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) amemtaka Mkuu wa Polisi wilayani hapa (OCD), Gires Muroto, kuachia ngazi baada ya kuzuia mikutano yake.

Lema alimtaka OCD huyo kujitoa kwenye uongozi wa Jeshi la Polisi na kwenda kufanya kazi ya uenezi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Lema alisema Aprili 22 mwaka huu aliandika barua ya kuomba ulinzi kwenye mikutano yake.
OCD huyo alifuta mikutano ya shughuli za mbunge huyo aliyoiruhusu kwa kigezo kuwa alipokea maombi mengine ya CCM kufanya mkutano eneo alilotaka kufanya mkutano.
Lema alisema Aprili 23 alipokea barua ya OCD ikimzuia kufanya mkutano kwa hoja kwamba kuna tishio la usalama jijini Arusha kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea kwenye baa ya Arusha Night Park, hivyo hawaruhusu mikusanyiko.
“Mimi ni mwakilishi wa wananchi wa Arusha, watu wangu wamepigwa mabomu, nataka nizungumze nao niwatie moyo nazuiwa… wiki ijayo naenda kwenye kikao cha Bunge la Bajeti, nataka niwasikilize wananituma nikawasemee nini sipewi ruhusa, nataka nisikilize kero za wapiga kura wangu OCD ananizuia.
“Hivi tukimaliza hapa kama madereva wanaogopa kuendesha gari kutangaza mkutano, kazi hiyo nitaifanya mwenyewe, huu ni uhuni kwa sababu kuna mikutano ya injili inaendelea, ibada zinafanywa makanisani na misikitini, masoko ambayo ndiyo yenye mikusanyiko mikubwa inaendelea.
“Kumbi za starehe tena za usiku zinafanya kazi kama kawaida, hata hapo palipopigwa bomu watu wanakusanyika, kwanini mkusanyiko wa mbunge na wananchi wake ndiyo unaonekana kuhatarisha usalama?” alihoji Lema.
Alisema sheria ya kinga, haki na madaraka ya Bunge inamruhusu kuzungumza na wananchi wake kwa uhuru, na yeyote atakayejaribu kumzuia atatenda kosa na anapaswa kushitakiwa.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leberatus Sabas, alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo, alijibu kwa mkato: “Tayari tumeshalimaliza suala hilo, tumeruhusu mikutano yake.”
Awali Aprili 17, mwaka huu, Lema alimwandikia barua OCD akiomba kufanya mikutano ya wananchi kwa nafasi yake kama mbunge kwenye kata za Levelosi, Terrat, Daraja Mbili na Moshono kwa tarehe tofauti.
Lema alisema kuwa siku hiyohiyo alipokea barua toka kwa OCD akimruhusu kuendelea na mikutano yake, lakini katika hali isiyo ya kawaida, Aprili 20, akapokea barua nyingine kutoka kwa kiongozi huyo wa polisi akizuia mikutano hiyo kwa maelezo kuwa Aprili 19, mwaka huu CCM nao wamepeleka barua wakiomba kufanya mikutano maeneo hayo jambo wanaloona linaweza kusababisha uvunjivu wa amani.
Lema amjibu JK
Katika hatua nyingine, Lema amemtaka Rais Jakaya Kikwete aelewe kuwa maandamano ya Jiji la Arusha husababishwa na watendaji wa serikali yake kupindisha sheria na kuminya haki za umma, hivyo huwalazimu kuandamana ili kuzidai.
Alisema kuwa hategemei kusifiwa na kiongozi huyo wa nchi katika harakati zake za kupigania haki ya wananchi wake na siku ikitokea anamsifu, itabidi ajitathmini ni wapi amekosea.
Lema alisema jambo la kusikitisha ni kuwa wale wanaohusika na uvunjivu huo wa sheria na haki za binadamu ni kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, na wote wamepandishwa vyeo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post