Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Watanzania wasomao Beijing
China, Bw. Shija Nobeji akitoa maelekezo ya namna ya kupiga kura kwenye zoezi
hilo. Wengine katika picha ni wajumbe wa kamati yake.
Watanzania wasomao Beijing, China wakifuatilia kwa makini mwenendo
wa zoezi la uchaguzi wakati Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi akitoa maelekezo.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wakiwa katika tabasamu lenye
bashasha muda mfupi kabla ya kumwaga sera zao. Kutoka kushoto ni Joel Kayombo,
Eusebia John na Suleiman Serera.
Mdau Majura Sospeter aka Mayor wa Jiji la Beijing akitimiza haki
yake ya kikatiba kuwachagua viongozi wa Umoja.
Kamati ya uchaguzi ikihesabu kwa umakini kura za wagombea ili
kuhakikisha uchakachuaji hauwi sehemu ya mchakato.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Bi. Nassra Nassoro
Suleiman akitangaza matokeo ya uchaguzi huo ambapo alimtangaza Suleiman Serera
kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Watanzania wasomao Beijing, China.
Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Watanzania wasomao Beijing, China Bw.
Suleiman Serera (aliyevaa suti) akitoa pongezi kwa watanzania mara baada ya
kuchaguliwa kuwa mshindi. Wengine kutoka kushoto ni Liberatha Rushaigo (Naibu
Katibu Mkuu), Mnemo Saleh (Makamu mwenyekiti), Olivo G. Mtung'e (Katibu Mkuu)
na Khamis Khalid Said (mtunza hazina)
Mwenyekiti mpya Suleiman Serera akishikana mkono na Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake Bw. Daninga Philip. Wengine katika picha ni uongozi mzima
wa Watanzania wasomao Beijing.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Umoja wa wanafunzi wanaosoma
Beijing, China (TzBeijing ) Bw.Philip Daninga akiongea na wanachama wa umoja
huo muda mfupi kabla ya zoezi la kupiga kura lililofanyika mwishoni mwa wiki
hii kwenye Ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania, China. Wengine katika picha kutoka
kushoto ni Bw. Eusebia John (Makamu Mwenyekiti) na Suleiman Serera (Kaimu
Mhasibu)
Umoja
wa watanzania wasomao Beijing China (TzBeijing) mwishoni mwa wiki
walifanya uchaguzi wa viongozi wao unaotazamiwa kudumu kwa mwaka mmoja
ambapo Suleiman Serera aliibuka kidedea kwa kuzoa kura 27 kati ya 41
zilizopigwa na hivyo kutangazwa rasmi kuwa mwenyekiti mpya wa umoja
huo.
Wagombea
wengine wa nafasi hiyo walikuwa ni Joel Kayombo aliyepata kura 6 na
Eusebia John aliyeambulia kura tatu.
Wagombea wengine walioibuka kidedea na nafasi zao katika mabano ni
pamoja na Mnemo Saleh (Makamu mwenyekiti), Olivo G. Mtung'e (Katibu
Mkuu), Liberatha Rushaigo (Naibu Katibu Mkuu) na Khamis Khalid Said
aliyeshinda nafasi ya utunza hazina.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi Serera alisema kwamba kazi
iliyoko mbele yake ni kuwaunganisha watanzania wote jijini Beijing na
kuhakikisha umoja huo unakuwa imara na wa mfano katika kujenga taswira
nzuri ya Tanzania.
Awali
kabla ya uchaguzi huo wa kwanza na wa aina yake, iliwekwa mikakati ya
kabambe ya maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar ambapo burudani kemkem kutoka kwa wanafunzi hao zinatarajiwa
kupamba tukio hilo la kihistoria