Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai cp Issaya Mngulu akiongea na waandishi wa habari hivi leo amesema kuwa mlipuko uliotokea juzi katika bar ya Arusha Night park(Matako bar) ulikuwa ni wabomu la kutengenezwa kienyeji
Amesema kuwa katika tukio hilo la bomu watu kumi na tano walijeruliwa na walifikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mounti meru lakini mpaka sasa watu wat u saba wameruhusiwa na wengine nane bado wamelazwa katika hospita hiyo hiyo ya mkoa
Aidha ameongeza kuwa jeshi la polisi limekamata kitu ambacho kinasadikiwa ni kifaa cha kutengenezea bomu ambacho kimekutwa kimetelekezwa katika bar moja inayojulikana kama washngton bar ilipo jijini hapa.