Na Mwandishi Wetu
Warembo watakaoshiriki kwenye
kinyang’anyiro cha kusaka malkia wa Tabata, Redds Miss Tabata 2014,
watatambulishwa siku ya sikukuu Pasaka
katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo
Joseph Kapinga amesema jana kuwa utambulisho huo utaenda sambamba na uzinduzi
wa Miss Tabata 2014.
Kapinga alisema kuwa wapenzi
wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla ya kushiriki
kwenye shindano la Redds Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni wa
mwezi ujao.
Katika uzinduzi huo warembo
hao watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
Pia watakuepo viongozi
waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na
Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa.
Kapinga alisema washiriki 21
wanaendelea na mazoezi ya Miss Tabata kila siku katika ukumbi wa Da West Park
chini ya wakufunzi watatu - Neema Chaki,
Pasilida Bandari na Bokilo.
Warembo hao ni Esther Frank
Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias
Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18), Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi
(20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wengine ni Annatolia Raphael
(21), Mary Henry (21), Evodia Peter
(22), Fatma Hussein Ismail (20), Ester
Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles
Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20).
Warembo watano kutoka Tabata
watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo anayeshikilia taji la
Miss Tabata ni Noela Dorice Mollel ni
Redds Miss Ilala.
Miss Tabata inaandaliwa na
Bob Entertainment na Keen Arts.