Tatizo la ukosefu wa maabara ya masomo ya sayansi katika shule ya
sekondari ya Malula iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha umetajwa kama tatizo
la wanafunzi shuleni hapo kutopenda masomo hayo hali inayochangia ufaulu mdogo
katika mitihani yao.
Hayo yalisemwa na mkuu wa shule hiyo,Rehema Mroso wakati
akishiriki zoezi la ujenzi wa msingi wa maabara ya masomo hayo ulioanza hivi
karibuni kwa kuwashirikisha wanafunzi pamoja na viongozi wa serikali ya kijiji
inayoizunguka shule hiyo.
Akihojiwa na gazeti hili wakati zoezi hilo likiendelea mkuu
huyo wa shule alisema kuwa pamoja na wanafunzi wengi shuleni kupenda masomo ya
sayansi lakini tatizo la ukosefu wa maabara shuleni hapo umechangia kwa kiasi
kikubwa baadhi yao kukimbia somo hilo.
Hatahivyo,Mroso alisisitiza kuwa ujenzi wa mabara hiyo
unaotaraji kugharimu kiais cha zaidi ya sh,80 milioni unaotaraji kukamilika mwishoni
mwa mwaka huu huenda ukawa ufumbuzi wa tatizo hilo ingawa sio kwa kisi kikubwa.
“Ujenzi huu wa maabara utasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi
wangu kupenda masomo ya sayansi “alisema Mroso
Hatahivyo,baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji
inayoizunguka shule hiyo walibainisha ya kwamba kukamilika kwa ujenzi huo
unategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwa wazazi wa wanafunzi shuleni hapo na
kuwataka kuchangia kwa nguvu zao michango ya fedha ili kumaliza zoezi hilo.