Mwenyekiti wa Umoja Asasi za Kiraia, Bw. Irenei Kiria akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Tathimini zilizofanywa na asasi za kiraia kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba mpya unaoendelea katika Bunge la Katiba mjini Dodoma, Katika tahimini yao hiyo, umoja huo umegundua madhaifu mengi sana ambayo kama hayatapatia ufumbuzi wake basi katiba mpya yenye kumjali mtanzania ni Ndoto kupatikana. Pembeni ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi Kijo Bisimba.
Baadhi ya Wanachama wa Asasi za Kiraia (AZAKI), wakifuatilia kwa makini.
Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko hilo.
Kila mmoja akifuatilia kwa karibu...
Tupenda kuipongeza serikali na hasa kumongeza kwa dhati Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kukubali kuansiha mchakato wa kutunga katiba mya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunalishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutunga sheria zote zinazowezesha kuelekeza hatua mbali mbali za mchakato huu.
TUnaishukuru Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Uongozi wa Jaji Joseph Sinde Warioba kwa kuendesha zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa wananchi na kuandika rasimu ya kwanza nay a pili za Katiba Mpya.
Tunawashukuru wananchi, wataalamu na Asasi mbali mbali kwa kushiriki na kutoa maoni katika hatua mbali mbali za mchakato huu wa kutunga Katia Mpya.
Kutokana na namna mambo yananvyokwenda katika Bunge Maalum la kutunga Katiba, Asasi za Kiraiaziliona umuhimu kukutana kuanzisha tarehe 8 Aprili 2014 kutafakari yanayojiri na kukubaliana utakuwa mchango wa Asasi katika kuhakikisha Tanzania inapata katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na ya vizazi vijavyo. Baada ya vikao vya mara kwa mara na majadiliano mengi pamoja na kukusanya taarifa kadhaa. Hatimaye katka kikao cha tarehe 15 Aprili 2014 tulikubaliana tamko.
Kwa hiyo sisi Asasi za Kiraia tumekubaliana ya kwamba:
Kwa kuwa huu ndiyo mchakato pekee hapa Tanzania wa kutunga katiba mpya ambao umewahusisha wnanchi tangu hatua za awali, tunauunga mkono na kuutakia mafanikio.
Kwa kuwa Rais wa Jamhuri wa Tanzania amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha katiba mpya inapatikana kabla ya kipidi chake cha uongozi kuisha, ni vema Bunge Maalum la Katiba likazingatia yafuatayo;
1. Sisi Asasi za Kiraia tunaunga mkono Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama ilivyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kwa kuwa imekidhi mahitaji ya Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo kama ikipita itaimarisha uadilifu, uwazi, uwajibikaji, amani na umoja wetu.
2. Kwamba hatujafurahishwa na mijadala ndani ya Bunge Maamul la Kutunga Katiba mijadala ambayo imepoteza utaifa na badala yake imejikita kwenye kutoheshimiana, ubabe, ubaguzi, vijembe na vitisho.
3. Kwamba tumehuzunishwa sana na tabia ya kudhihakiana na kudharau Rasimy ya pili ya Katiba pmoja na tume ya mabadiliko ya katiba na hasa Mwenyekiti wake.
4. Tunaona kwamba mwennendo wa mijadala ni kuelekea kutetea maslahi ya watawala wa vyama vya siasa badala ya maslahi ya utaifa na ustawi wa wananchi.
5. Kwamba kitendo cha baadhi ya wajumbe kupendekeza kutoa maneno; uwajibikaji, uadilifu, uwazi katika kipengele cha tunu za taifa inatia mashaka kama nia ya Bunge Maalum la Katiba ni kutuletea katiba itakayotutatulia matatizo hayo.
6. Kwamba hatufurahishwi na malumbano yasiyo na tija yanayochukua muda mrefu kwenye mambo madogo madogo. Hii inapelekea kupoteza muda na hivyo kutumia rasilimali za umma vibaya.
7. Kwamba hatujafurahishwa na kufungwa kwa tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Na pia hakuna juhudi za serikali kuwafikishia wananchi Rasimu ya Katiba mpya na kuwaelimisha maudhui yake.
8. Tumeelewana kwamba tulikosea kutuga sheria inayohusu wabunge wa kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la katiba. Kwa kawaida watatetea maslahi yao kwanza kabla ya maslahi ya wananchi. Mfano bunge la Tanzania lina wabunge 357, lakini rasimu inapendekeza wabunge 75 tu. Hili ni tishio la wazi kwa maisha ya kisiasa ya baadae ya wabunge madalakani sasa na hivyo wanapata umoja wa kupambana kuhakikisha rasimu hii isipate ka ilivyo.
9. Tunaelewa pia kwamba, Rasimu hii imependekezwa kupunguza madaraka ya Rais ya kuteua viongozi na watendaji wa serikali. Jambo hili, kwa mtazamo wetu ni tishio kwa wagombea urais kwamba hawatakuwa na nguvu ya kuahidi wapambe wao nafasi za uteuzi ili wawaunge mkono kwenye kampeni ya uchaguzi.
Rai yetu Umoja wa AZAKI.
Tunasihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Uongozi wa Bunge hilo kurekebisha hizo kasoro walizozieleza.
Irenei Kiria
Mwenyekiti wa Umoja wa Asasi za Kiraia (AZAKI).