Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David A. Misime - SACP akiongea na wanahabari
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu
watatu kwa kosa la Kupatikana na Bhangi kiasi cha Kilogramu 133.5 yenye thamani
ya Ths. 20,025,000/= bei ya mitaani (street value). Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe 16/04/2014 majira ya
7:30 mchana eneo la Stend Kuu ya mabasi katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma.
Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha Bhangi katika mabegi baada ya kupanda
basi kutokea Kijiji cha MANONGA – TINDE Mkoani SHINYANGA kwenda jijini Dar es
Salaam katika basi namba No. T.931 CGU mali ya kampuni ya NEW FORCE linalofanya
safari zake kutokea Kahama kwenda jijini Dar es Salaam. Watu hao walifahamika
kwa majina ya:-
1.
CALVIN S/O
PROSPER SALEKA, miaka 23, kabila Mchaga, Mwanafunzi wa chuo cha Institute of
Finance Management (IFM) cha Dar es Salaam, mwaka wa pili, alikamatwa akiwa na
mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 51kgs
2.
JOHN S/O JOSEPH,
Miaka 31, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam,
alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito wa 42.5kgs.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
3.
JOSEPH S/O
CHARLES BATONI, Miaka 22, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa Shinyanga.
alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 36.5kgs
Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia taarifa za raia
mwema aliyewatilia mashaka na kutoa taarifa Polisi. Mbinu waliyotumia
kusafirisha ni kuhifadhi katika mabegi makubwa ya nguo na kufunga kwa mifuko ya
nailoni kisha kusaga vitunguu na kuweka katika mabegi hayo pamoja na kupulizia
manukato (perfume) ili kuondoa harufu wasiweze kugundulika kirahisi.
Tukio lingine katika kijiji cha Central Kiteto Tarafa
ya Mlali Wilaya ya Kongwa zilikamatwa lita 300 za Pombe haramu ya Gongo nyumani
kwa Salumu s/o Chamagulu ambaye alikimbia baada ya kuona Polisi na tunaendelea
kumtafuta.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi David A. Misime – SACP, anawapongeza kwa dhati raia wema
wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili
kuendelea kudhibiti madawa ya kulevya na Pombe ya Moshi inayoharibu vijana
wengi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia