Kikundi cha ngoma kikitoa Burudani kabla ya pambano la Ngumi kuanza kati ya Bondia Alibaba Ramadhan wa Kilimanjaro na Roy Mbunda wa Ruvuma. |
Mgeni rasmi katika pambano hilo mkuu wa polisi wa wilaya OCD Deusdedit Kasindo akizungumza kabla ya kuanza kwa pambano la ngumi katika ya bondia Alibba na Roy Mbunda. |
Mwakilishi wa kampuni ya Panone ,Gido Marandu akizungumza kabla ya pambano hilo. |
Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akizungumza kabla ya pambano hilo. |
Mmoja wa mabondia waliopambana katika mapambano ya utangulizi akitokwa mchuzi baada ya kuchezea masumbwi toka kwa Bondia Mwakipesile. |
Bondia Mwakipesile(Shoto) akisukuma konde . |
Hatimaye bondia Mwakipesile akaibuka mshindi kwa pointi |
Likafuata pambano la Bondia Massawe toka kibosho . |
Akapambana na Bondia Rasta toka jijini Arusha. |
Bondia Rasta akachezea ngumi za kutosha toka kwa Mkibosho.Masawe. |
Bondia Rasta akaomba Poooo.akasalimu amri akasema siendelei na pambano taumia. |
Bondia Masawe toka Kibosho akapewa Ushindi kwa kumtwanga KO Bondia Rasta. |
Likafuatia pambano kali tena na hapa ni kati ya Fredy George kutoka Himo mwenye Bukta ya njano na Pascaly Bruno wa Moshi. |
Ngumi zikapigwa kwa raund zote nne. |
Mabondia wote wakiwa hoi kama anavyoonekana Fredy George akivuliwa Groves. |
Bondia Pascaly Bruno akatangazwa mshindi . |
Baadae sasa likafuata pambano lililokuwa likisubiriwa na wengi ni la kuwania mkanda wa taifa kati ya Bondia Alibaba Ramadhan na Roy Mbunda. |
Bondia Alibaba Ramadhan akiingia ukumbini akiwa anasindikizwa na wapambe wake. |
Bondia Alibaba akipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa pambano. |
Pambano likaanza ndani ya round ya pili tu Bondia Alibaba anasukuma konde kwa bondia Roy Mbunda lililompeleka chini. |
Baadae Roy Mbunda akaamka akigugumia maumivu ya mguu akidai msuli wa paja umebana. |
Mwamuzi wa pambano hilo Said Chaku akalazimika kutaka kufahamu endapo Mbunda ataendelea ama la. |
Mwamuzi Chaku akalazimika kukatisha pambano kutokana na Bondia Mbunda kuda hatoweza endelea na pambano. |
Roy Mbunda akisikilizia maumivu. |