Mkurugenzi wa Tanzania Horticulture Association(TAHA) bi,Jackline Mkindi
akizungumza na vyombo vya habari ambao hawapo pichani juu ya maonesho
ya kilimo ambao yanatarijiwa kufanyika siku ya Aprili 25 na 26 katika
viwanja vya AVRDC vilivyopo eneo la Tengeru wilayani arumeru mkoani
arushakilia kwake ni Mratibu wa Agri-Hub Tanzania bw,Tom ole sika
Waandishi wa habari wakiwa wanafatilia taarifa iliyokuwa inatolewa na afisa mtendaji mkuu wa Taha
WAKULIMA na wafanyabiashara za kilimo zaidi ya 500 kanda
ya kaskazini mwa Tanzania wanatarajiwa kukutanishwa na taasisi za kifedha 48 ili
kuweza kuongeza ufahamu na uelewa juu ya huduma mbalimbali za nkifedha
zitolewazo na mabenki,taasisi ndogo ndogo za kifedha,mashirika ya bima,taasisi
za elimu na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza
na vyombo vya habari afisa mtendaji mkuu
wa TAHA bi.Jackline Mkindi amesema kuwa wakulima wadogo wadogo wamekukwa
wakikabiliwa na changamoto kubwa ya ya upatikanaji wa huduma za kifedha
hususani kwa wadau wa sekta ya kilimo.
Katika kutatua
changamoto hiyo ya mitaji Agri-Hub Tanzania ikishirikiana na TAHA
mashirika,asasi mbalimbali kwa umoja wao
wamethamiria kuwaunganisha wadau wa kilimobiashara na watoa huduma za kifedha
moja kwa moja ili pande zote mbili ziweze kukuelewana na juu mahitaji yao na
hatimaye watoa huduma za kifedha waweze kubuni huduma bora zaidi za kuimarisha
utoaji huduma zao kwa wadau wa kilimo.
Mkindi alisem
kuwa maonesho hayo yatakwenda sambamba na uwasilishwaji wawa mada mbalimbali
ikiwemo uaandaaji bora wa wa mpango biashara (business plans),umuhimu wa wa
soko la hisa katika kuhakikisha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu na matumizi bora ya mikopo
katika biashara hususani za kilimo.
Naye mtaribu
kutoka kampuni ya Agri-Hub Tanzania bw,Tom Ole Sikar,alisisitiza kuwa maonesho
hayo yanalenga kuwawezesha wakulima wajasiriamali pamoja na wamiliki wa
biashara za kilimo kama wachuuzi,wauzaji wa pembejeo na wasindikaji kutambua
fursa mbalimbali za mitaji na usalama wa kifedha(Financial security) zilizopo
kwa biashara za kilimo.
Aidha sikar
alisema kuwa wadau hao wataweza kuunganishwa na taasisi muhimu za fedha ikiwa ni pamoja na kushiriki katika
mawasilisho na majadilino juu ya fursa za sekta binafsi katika kilimo pamoja na
wataalamu wa mambo ya fedha na watoa huduma za maendeleo ya biashara kupitia
semina zitakazotolewa sambamba na maonesho hayo.
‘’maonesho
hayo yatawawezesha wadau kutambua njia za kuboresha biashara na utoaji wa
huduma kwa walengwa ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka kwa wafanyabiashra
wengine wa kilimo waliofanikiwa kutembelea maonesho “alisema bw,Sakar
Maonesho
hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Taasisi ya AVRDC(The World Vegetable
Centre) kuanzia tarehe 25 na 26 april
kuanzia majira ya saa tatu aubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia