TATIZO LA UHABA WA MAFUTA LAAMIA ARUSHA

tatizola ukosefu wa mafuta katika sheli nyingi limeingia jiji Arusha na leo katika sheli nyingi zimeonekana kuwa na foleni kubwa huku nyingine zikiwa zimefungwa kutokana na tatizo la kuishiwa mafuta

katika baadhi ya sheli ambazo libeneke la kaskazini limeshuhudia misafara ya magari mengi ambayo yanataka mafuta ,pamekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa madereva kwani wamedai kuwa mafuta yamepandishwa na pia wamekuwa wanauziwa kwa mashariti kuwa ,kila gari litauziwa mafuta ya shilingi elfu kumi tu na sio zaidi ya hapo.

watu wengine wamelazika kupaki magari yao nyumbani kutokana na tatizo hili la kutokuwa na kukosa mafuta ya magari yao

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post