Ticker

6/recent/ticker-posts

NSSF YASIFIWA KWA KUTOA HUDUMA BORA


Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la NSSF. Kulia ni  Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Katavi, Anna Lupembe.
Naibu Waziri wa Fedha akipata maelezo ya shughuli za NSSF.
Mmoja wa wanachama wa NSSF akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa hiari wa kuchangia mafao.   
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiangalia mchoro wa jengo la Hospitali ya Apollo itakayokuwa ikitoa matibabu ya magonjwa ya moyo pamoja na Chuo cha Utabibu na Dawa eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimpa maelezo kuhusiana na hospitali hiyo. 
Wengi walivutiwa na huduma za NSSF.
Huduma za matibabu.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene  akizungumza na waandishi wa habari.
Watu wengi walijitokeza katika banda NSSF.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi, Anna Lupembe.
Baadhi ya watoto waliotembelea banda la NSSF wakipata zawadi ya madaftari kutoka kwa Ofisa wa NSSF, Silvia Mashuda.
Wateja wa Sh,irika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakisubiri kupata huduma katika banda la shirika hilo katika viwanja vya Sabasaba.

Na Mwandishi Wetu



NAIBU Waziri wa Fedha, Janet Mbene amesema lengo la kuzitembelea taasisi za kifedha na nyingine zilizoko chini ya Wizara hiyo ni kutaka kujua mafanikio na changamoto za taasisi hizo.

Mbene amesema hayo wakati alipotembelea banda la maonesho la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Alisema baada ya kutembelea na kuangalia banda hilo, alibaini kuwa changamoto kubwa ni fedha ambazo zinahitajika kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za mfuko huo, kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Mbene alisema baada ya kubaini hayo serikali inao wajibu wa kutafuta kila njia lengo likiwa ni kuzipatia ufumbuzi wake.

Unajua hivi sasa kila kazi zote zinafanywa kwa kutumia mfumo wa teknolojia ambao kwa kawaida ni mahususi katika kurahisisha kazi na kuifanya iwe bora zaidi”alisema Mbene.

Mbene alisema ukiachilia mbali uhitaji wa teknolojia bado pia wataalam ambao wangetumika kusimamia mifumo hiyo hawatoshi, serikali kwa kuliona hilo itahikikisha kuona wanapatikana.

Akizungumzia kuhusu mafanikio ya Mfuko wa NSSF, Eunice Chiume alisema mfuko huo hivi sasa umepiga hatua katika kuwafikishia huduma mbalimbali wateja wake kila kona ya nchi na nje.

Aidha, Mfuko huo katika kuboresha maisha ya wafanyakazi wake inatoa mikopo, hata hivyo masharti ya kupata mkopo huo ni lazima muombaji awe mwanachama wa SACCOS.

Mbene aliongeza kuwa SACCOS itawajibika kupokea maombi iwapo SACCOS hiyo imesajiliwa kikamilifu na imeendesha shughuli zake kwa kipindi cha miaka mitatu na si chini ya hapo.

Post a Comment

0 Comments