Wanamgambo
wa kiislamu, Boko Haram wamekuwa wakitekeleza mashambulizi kadha wa
kadha ya mabomu na mauaji nchini Nigeria tangu walipoanza Operesheni yao
mwaka 2009 wakiwa na nia ya kuunda nchi ya kiislamu. Boko Haram
huwashambulia viongozi wa kiislamu ambao hukosoa misimamo yao.
Jeshi la
polisi nchini Nigeria limetoa taarifa ya kuuawa takriban watu 25
kutokana na mlipuko wa bomu ulio tokea leo jioni katika barabara ya Isa
Kaita mjini Kaduna.Bomu hilo lilimlenga Kiongozi wa dini ya kiislamu
mwenye msimamo wa wastani Dahiru Bauchi ambaye alikua akitoka kuhubiri
katika viwanja vya Murtala Muhammed. Bauchi amenusurika katika shambulio
hilo, hajajeruhiwa halikadhalika bado haijajulikana waliofanya
shambulio hilo.