Sheikh
wa Msikiti wa Qiblatan,Sood Ally Sood (37) uliopo Kilombero jijini
Arusha amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono alipokuwa akila daku
nyumbani usiku wa kuamkia jana.
Pamoja
na Sheikh Sood, mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa kwa
jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam pia
amejeruhiwa katika tukio hilo na wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa
ya Mount Meru kwa matibabu.
Sheikh
alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha
makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote.
Akizungumza
hospitalini hapo, Sheikh, Sood alisema tukio hilo lilitokea nyumbani
kwake eneo la Majengo ya chini, usiku wa kuamkia jana saa 5:00 wakati
yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni.
“Nikiwa
sijui hili wala lile nilishtushwa na mlipuko ulioambatana na vyuma
mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa
ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika
kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumba tulichokuwamo,” alisema
Sheikh Sood.
Alidai
anawajua waliotekeleza shambulio hilo kwa sababu amekuwa akipokea
vitisho kutoka kwa watu anaowafahamu na tayari alikuwa ametoa taarifa
kwa vyombo vya dola.
Alisema
kuwa siku tatu kabla ya tukio hilo alikoswakoswa kupigwa risasi na watu
wasiofahamika wakati akitoka msikitini na akatoa taarifa Kituo Kikuu
cha Polisi jijini Arusha kuhusu tukio hilo. Sood anasema kuna baadhi ya
vijana anawatuhumu juu ya matukio hayo.
Sheikh
huyo ambaye ni Kiongozi wa dhehebu la Answar sun Kanda ya Kaskazini
amekuwa akitofautiana na waumini wenzake kutokana na msimamo wake wa
kutokukubaliana na baadhi ya waumini wenye msimamo mkali wa msikiti huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alikemea matukio ya mabomu
yanayolitikisa Jiji la Arusha katika siku za karibuni na kuviagiza
vyombo dola kufanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wote ili hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yao.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha tukio hili limetekelezwa na watu walio karibu na
Sheikh. Polisi wanaendelea na uchunguzi kwa sababu baadhi ya watu
wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili pia ni miongoni mwa watuhumiwa
kwenye matukio mengine ya milipuko ya bomu Arusha,” alisema Mulongo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabasi alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa majeruhi wanaendelea vyema huku polisi
wakiendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika.
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema alielezea kusikitishwa na matukio ya
milipuko ya mabomu Arusha na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi
wa kina kuwakamata wahusika bila kujali vyeo, nyadhifa, dini, itikadi
wala rangi zao. Kinyaiyas Blog inajiuliza haya mambo ya kulipuana kila
kukicha na haswa mkoani Arusha yataisha lini wkt nchi yetu na watu wake
hatujazoea hayo mambo jamanii...
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia