Ticker

6/recent/ticker-posts

TASWIRA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA MKOA WA MWANZA.


Askari wa parade akimkabidhi mkuki na ngao mwakiliashi  wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, kwaajili ya uwekaji wa silaha za asili kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, akiweka silaha za asili kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe. Anthony Diallo, akisali mara baada ya kuweka silaha za asili za upinde na mshale, kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza
Mwakilishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Mr. Mkabenga, akiweka shoka kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Mwakilishi toka kanisa la Roman Catholic akiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza
Wawakilishi toka watu wa madhehebu ya Hindu Union wakiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Masunga akiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza
Wimbo wa Taifa ulipigwa.
Wadau mbalimbali wamehudhuria katika maadhimisho haya muhimu.
Wadau mbalimbali wamefika hapa ili kushiriki Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa, yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Eneo la tukio.
  chanzo; gsengo blog

Post a Comment

0 Comments