Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea kwa
mara ya pili maonesho ya kimataifa ya bishara katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, baada ya ratiba yake
kutokamilika katika ziara yake aliyoifanya siku ya Jumamosi kutokana na
muda. Na kama ilivyo ada wananchi walifurahi kuwa naye karibu kama
ambavyo yeye pia alifurahi kujumuika nao kwenye maonesho hayo ya kila
mwaka. Watoto ndio waliokuwa wakimvutia zaidi Rais Kikwete ambapo kila
mara alisimama na kuwasalimia.