mkuu wa wilaya ya Arumeru munasa nyirembe akiwa anongea na waandishi wa habari
picha ikionyesha wa kwanza kushoto mkurugenzi wa vitambulisho vya taifa
ofisi ya zanzibar Vuai
Sueleiman akifuatiwa katika kati mkuu wa wilaya ya Arumeru pamoja na
mkurugenzi wa Nida taifa Dickson Maimu wakiimba wimbo wa umoja
picha ikionyesha washiriki wa mkutano huo wakiwa wanasikiliza kwa
makini mkuu wa wilaya wakati akiongea katika ufunguzi wa mkutano huo
washiriki katika mkutano wa Wafanyakazi wa Mamlaka
ya vitambulisho vya taifa NIda wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni
rasmi mkuu wa wilaya ya arumeru Munasa Nyirembe leo nje ya jengo la
hotel ya Snowcrest sehemu ambayo mkutano ulikuwa unafanyika
Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ,
Dickson Maimu akiwa anaongea na waadhishi wa habari kuhusiana na zoezi lima la ugawaji wa kitambulisho cha taifa
picha ikionyeshoamkuu wa wilaya ya Arumeru munasa nyirembe akiwa anateta jambo na mkurugenzi wa NIDA pamoja na washiriki wengine
washiriki wakiwa wanabadilishana mawazo na mkurugenzi wa vitambulisho
vya taifa zanzibar aliyevaa kibaraka shia mara baada ya kutoka kwenye
ufunguzi wa mkutano
Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ,
Dickson Maimu amesema kuwa zoezi la usajili wa watu na kuwapatia
vitambulisho hivyo litaanza katika mikoa
ya Lindi,Mtwara na Pwani hivi karibuni
hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa baada ya kukamilisha
zoezi hilo katika mikoa ya Dar es Salaam na mikoa yote mitano ya Zanzibar sasa
wanaelekea katika mikoa hiyo .
Akizungumza katika mkutano wa Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo unaoendelea jijini hapa alisema kuwa
vitambulisho hivyo vitawasaidia Watanzania kukopesheka kwa urahisi baada ya
kutambulika hivyo kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa Ujumla,pia
kuwatambua wageni na wakimbizi.
Maimu amesema kuwa serikali imetenga fedha za kutosha katika
bajeti kiasi cha shilingi bilioni 200
ambazo zitasaidia kufanikisha zoezi hilo na kulikamilisha,tunatarajia baada ya mikoa hiyo itafuata Kilimanjaro,Arusha na
Tanga.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha ,Nyirembe Munasa
alisema kuwa licha ya vitambulisho hivyo kuwasaidia wananchi kiuchumi
vitawasaidia katika masuala ya ulinzi na usalama ,kutatusaidia kuwatambua
wachafuzi wa amani inawezekana wanatoka nje pia kudhibiti ugaidi.
Nyirembe ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa inatoa elimu
ya kutosha kwa wananchi kwa kupitia vyombo vya habari na taasisi mbali mbali
zikiwemo shule na vyuo ili watanzania wajue umuhimu wa vitambulisho hivyo .
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo kwa upande wa Zanzibar,Vuai
Suleman alisema kuwa tayari zoezi hilo limekamilika katika nchi hiyo yenye
mikoa 5 na wilaya 10.amewataka watanzania kutoa ushirikiano na kuwa na taarifa
muhimu ikiwemo kitambulisho cha mkazi,cheti cha kuzaliwa,vyeti vya kukupigia
kura ili kufanikisha zoezi hilo la kitaifa.