WATU
wanaosaidikiwa kuwa majambazi wameshambulia kwa risasi basi la Jeshi la
Magereza likiwa na watuhumiwa mbalimbali wakiwamo majambazi sugu na
kujeruhi askari wawili.
Habari
za uhakika zimeifikia hivi punde kuwa tukio hilo limetokea muda mchache
Jumatano Julai 2, 2014 eneo la Mikocheni karibu kabisa na hoteli ya
Regency, wakati basi hilo likiwa njiani kutokea mahakama ya Kawe
kurudisha watuhumiwa gerezani.
Askari
magereza walifanikiwa kuondoka na watuhumiwa hao na haijafahamika mara
moja hatima ya majambazi hao lakini askari mmoja amefariki kutokana na
hayo mapigano.
Jinsi tukio lilivyotokea
Shuhuda
mmoja anasema kuwa, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe
kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai
Kibaki road.
Hiyo
gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na
Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana, nyuma ya hiyo gari
ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.Gari ya magereza
ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari
ndogo mara ghafla tukasikia puu puuu poo pooo kama risasi 6 au 8
hivi,kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa
cha pesa na hakukuwa na escort yoyote.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni
wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja.
Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari
wake wakaiona hiyo inshu live,sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao'
majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa
risasi wale askari magereza.Askari magereza ile wanajiandaa kujibu
mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwa speed ya
220.
Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu,yaani ilikuwa kama Movie.