MOSHI mtangazaji wa habari za michezo wa Moshi FM radio iliyopo mkoani Kilimanjaro Henry Lyimo maarufu kwa jina la Kipese amefariki dunia jana usiku.
Kifo
chake kilisababishwa na ajali mbaya iliyotokea jana jioni maeneo ya
Mwika wakati Kipese akitokea Rombo katika majukumu ya kikazi akirudi
Moshi mjini. Ajali hiyo ilisababishwa na kugongana kwa pikipiki
aliyokuwa akiitumia Kipese na pikipiki nyingine ambayo haijafahamika kwa
haraka ilikuwa ya nani.
Kwa
sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kilema iliyopo
wilaya Moshi vijijini ukingojea utaratibu utakaofuata baada ya ndugu wa
Henry Lyimo kufanya maamuzi.
uongozi MZIMA WA blog ya libeneke la kaskazini unawapa pole sana ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.
Tags
MATUKIO HABARI