Wanafunzi wa shule ya awali wakiteta point za makundi yao kwa kubeba limao kwenye kijiko. huku mmoja wao akiwa nyuma akiokota baada ya kudondosha. |
Shule za sekondary wakitetea point kwa mchezo wa riadha. |
mchezo wa kuruka kwa gunia |
kujaza maji kwenye chupa |
kuvuta kamba kwa wazazi na walimu ambapo wazazi walishinda |
mkuu wa shule ambae ni muandaaji wa siku ya michezo hiyo |
kila mmoja alipokea zawadi kulingana na point zake |
meneja mauzo wa pepsi Ally alipokuwa akigawa zawadi kwa vikundi |
wanafunzi wa shule za awali nao walipata zawadi |
Na Bertha Ismail.
Katika hali
ya kukuza michezo mashuleni na kuinua vipaji vya wanafunzi shule ya Arusha Modern
imeendesha mashindano maalum kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa upande wa msingi
na sekondari ikiwa ni kuadhimisha siku ya michezo shuleni.
Katika
mashindano hayo yalihusisha makundi mbali mbali kutoka shule ya msingi na
sekondari ya Arusha modern, ambapo kila kundi lilishiriki michezo mbalimbali
ikiwemo Mpira wa miguu, mpira wa mikono, mpira wa pete, riadha, kukimbia kwenye magunia huku wazazi
na walimu kushindana kuvuta kamba.
Kwa upande
wa wanafunzi wa shule za awali wakishindana kujaza maji kwenye chupa ya
mililita 250, kupasua mapulizo sambamba na mashindano ya kuzunguka viti ambapo
kila kundi kupatiwa point za maksi
walizopata.
Mashindano
hayo yalihusisha kundi la Mandela team, Babro team, Nyerere team pamoja na
Einstean team ambapo kundi la Mandela lilifanikiwa kuzibwaga makundi pinzani 3
kwa kunyakua point 173 ikifuatiwa na Babro ikinyakua point 171 huku akijipatia
point 135 na kundi la Eistean ikijifuta machozi kwa point 110.
Akizungumzia
mashindano hayo, mkuu wa shule ya Msingi Arusha Modern Philip Wasike alisema
kuwa siku hii wameamua kuiadhimisha kwa mashindano hayo kutokana na kutambua
umuhimu wa michezo hasa kwa mwanafunzi anaetumia muda mwingi kusoma hivyo ni
lazima apate pia muda wa kupumzisha akili ili aweze kuelewa na kufaulu yale
anayoyasoma.
Maadhimisho
hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “michezo ni ajira” Wasike Alisema kuwa mbali na
hilo mashindano hayo wanakuwa wanaangalia vipaji vya wanafunzi wao ili kuweza
kuunda timu za kichezo mbalimbali na kuzishindanisha na timu za michezo hiyo
kutoka katika shule zingine za hapa jijini Arusha na mikoa mingine kwa ujumla.
“Kikubwa
tunachokifanya hapa ni kuangalia vipaji vya wanafunzi wetu ili kuunda timu za
mashindano na shule zingine ambapo tumeshapata baadhi ya majina ya wanafunzi
wanaofaa katika michezo mbalimbali hivyo tunachokifanya sasa ni kupeleka barua
za maombi katika shule zingine tuwe na mashindano ya hapa na pale angalau mara
moja kwa wiki au mwezi” Alisema wasike.
Kwa upande
wa wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Ally Ramoudh kupitia kampuni ya Pepsi
alisema kuwa kutokana na mvuto wa mashindano hayo na msisimko wake kwa
wanafunzi na kuvuta umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo kampuni ya Pepsi
itaendelea kudhamini siku hiyo ya michezo ili kufanikisha kukuza vipaji vya
wanafunzi hao na kufananishwa na wachezaji maarufu kitaifa na kimataifa kwani
shuleni ndio sehem ya nzuri ya kuonyesha kipaji na kukuzwa kwa urahisi.