SHAMRA
shamra za tamasha la Muziki wa Cigogo zitatarajia kulipuka hiyo kesho Julai 25,
kwenye kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa kwa kushuhudia vikundi zaidi ya
30, vikiwasha moto wa ngoma na muziki wa kitamaduni hu ku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema
Nchimbi akitarajiwa kulifungua rasmi.
Katika kukuza
na kuendeleza sanaa nchini, tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la msimu wa Saba
(7) likifahamika kama (Wagogo music festival 2014) lenye kauli mbiu
‘Utamaduni na Amani’ linatarajia kulindima kwa siku tatu, Julai 25 hadi
27, Kijijini hapo Chamwino Ikulu.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika mkutano
uliofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi
mkuu wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana, wa Kituo cha Sanaa Chamwino
(Chamwino Arts Center-CAC) alisema jumla ya vikundi 31 vinatarajiwa
kushiriki tamasha hilo.
“Tamasha
la Wagogo mwaka huu ni la saba, ambapo shamrashamra ya tamasha hilo zinatarajia
kuanza majira ya saa nane mchana Mkuu wa Mkoa atakapolifungua rasmi huku
tukitaraji pia kuwa na wageni wasiopungua 1000” alisema Dr. Kedmon Mapana.
Na kuongeza
kuwa, kituo hicho cha CAC kimekuwa
kikiandaa tamasha hilo kila mwaka huku lengo kuu likiwa ni kudumisha mila na
tamaduni za Wagogo.
Aidha,
alisema jumla ya wasanii 750 wanaotoka kwenye vikundi hivyo 31, wanatarajia watawasha moto wa aina yake kwa
kuonyesha sanaa ya muziki wa kabila hilo.
“Miaka ya
nyuma tulikuwa na vikundi vya kutoka hapahapa Chamwino na baadae kutoka ndani
ya Mkoa wetu pekee, lakini kwa sasa tumeamua kualika na makabila jirani.. wapo
wanaotoka Dar es Salaam, Pwani, Singida na Visiwani Zanzibar hivyo wote kwa
pamoja tutadumisha utamaduni wetu” alisema Dr. Kedmon Mapana.
Dk. Mapana
pia alipongeza wafadhili wakuu
wanalioliunga mkono tamasha hilo wakiwemo, Chamwino Connect na Schweizerische Eidgenossenschaft (German).
Tamasha
hilo pia uhudhuliwa na wageni mbalimbali kutoka mataifa ya nje, ikiwemo
nchi za Ulaya, America, Asia na bara la Afrika, ambapo pia kunakuwa na
warsha na makongamano katika vijiji vya Chamwino.
Aidha, alivitaja
vikundi vitakavyoshiriki tamasha hilo ni pamoja na kutoka Dodoma kuwa ni New Pendo,
Yelusalem, Inueni mioyo, Yeriko, Nyota njema, Ushirikiano, Nyerere na Ebenezer.
Vikundi
vilivyo vijiji vya Wilaya ya Chamwino ni Upendo (Kijiji cha
Dabalo), Imani, Sinai (Kijiji cha Membe). Mchungaji mwema,
(Kijiji cha Nzali), Juhudi, Muhubiri (Kijiji cha Kawawa), Nyota njema, Safina, Ndagwa
(Kijiji cha Msanga).
Msifuni
(Kijiji cha Mlimwa), Nyota, Ufunuo (Kijiji cha Majeleko), Simba (Kijiji cha
Mbele zungu) na Inueni mioyo (Kijiji cha Mgunga).
Vikundi
kutoka Wilaya ya Kongwa imani ( Kijiji cha Mkutani), Faru (Kijiji cha
Songambele) na Safina (Kijiji cha Chigwingili), Pia kikundi cha Uvuke
na Upendo (kutoka Manispaa ya Dodoma mjini).
Vikundi
vingine ni Mandoo/Tasuba kutoka Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Nazareti (Dar es
s Salaam), Muungano (Manyoni, Singida) na Zanzibar.
habari hii imeandikwa na Andrew Chale, Dodoma