Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na ujumbe kutoka Chuo
cha St. Thomas cha Marekani uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue JANA tarehe 16 Julai, 2014 amekutana na
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Thomas cha Minnesota, Marekani
wanaotembelea Tanzania kujifunza uzoefu wa Tanzania katika masuala ya
kiuongozi na anuwai ya tamaduni. Wanafunzi hao ambao kwa idadi yao ni
wanafunzi 14 wanaochukua Shahada za Uzamivu na Uzamivu katika masuala ya
Uongozi wa Kimataifa pamoja na Wakufunzi wao wawili, Dkt. Jean Pierre
Bongila na Dkt. Artika Tyner.
Mkutano
huu ni mwendelezo wa mkutano kama huu ambao Katibu Mkuu Kiongozi
aliufanya mwaka jana na kundi jingine la wanafunzi kutoka Chuo hicho
ambapo aliwapa uzoefu wa uongozi na anuwai ya tamaduni katika Tanzania,
Afrika na katika medani za kimataifa.
Kwa
kutambua umuhimu wa nasaha walizozipata wanafunzi wa mwaka jana, Chuo
hicho kiliomba na kukubaliwa fursa nyingine ya kuonana na Katibu Mkuu
Kiongozi. Ziara ya wanafunzi hao ilianzia Arusha tangu tarehe 12 Julai,
2014 na itamalizika tarehe 17 Julai, 2014.
Pamoja
na kupata fursa ya kuonana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa
wa Arusha, wanafunzi hao walipata pia muda wa kutembelea vivutio
mbalimbali vya utalii vilivyopo Arusha na baadaye Zanzibar. Na matarajio
ni kuwa wanafunzi hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania
sehemu mbalimbali za dunia watakakokwenda kufanya kazi.
Kwa
ujumla, wanafunzi wamepata fursa nzuri ya kuuliza maswali yaliyogusa
maeneo yote yanayohusu uongozi, siasa, uchumi, elimu, afya na utamaduni
ambayo yalipata ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia