Huku harakati za kutaka matumizi
ya Bangi kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani,
Tanzania haijaachwa nyuma.
Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa
Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria
ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.
Wanakijiji hao zamani walikuwa
wakitumia mbegu za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi
wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa wakihofia kukamatwa na polisi.
Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete
Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza
leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi
kukaanga na chakula.
Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.
Miti ya mimea hiyo pia ilikuwa ikitumiwa kutengeza kamba ambazo anasema zilikuwa za nguvu sana.
Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika wilaya hiyo.
CHANZO : BBC
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia