Muonekano wa lango kuu la kuingia ndani ya banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana kwa kupewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Utajiuliza kwani LG wapo ndani ya Banda la MeTL Group kwenye maonyesho ya Sabasaba kwa sababu MeTL Group wamekuwa Mawakala waliothibitishwa Tanzania nzima (Authorized Dealers) kuuza vifaa vya LG nchini. USISAHAU KUJINADIKISHA KWA AJILI YA DROO YA BAHATI NASIBU ITAKAYOCHEZESHWA TAREHE 7 MWEZI HUU NDANI YA BANDA LETU...!
Kampuni ya MeTL Group inahusika pia na masuala ya Vitenge, Khanga, Mashuka na n.k Njoo upendeze mwanamke na vitenge bora na imara kutoka MeTL Group.....Sikukuu ya Eid ilee na maandalizi yawe mapema kabisa...!
Wakazi wa jiji la Dar wakivinjari ndani ya Banda la Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL Group) kujipatia mahitaji mbalimbali za bidhaa bora kabisa kwa bei nafuu msimu huu wa Sabasaba.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiangalia na kupata maelezo ya bidhaa mbalimbali kama TV, Music System, Simu za mkononi za nyingine nyingi kutoka kampuni ya LG ambapo MeTL Group ndio Authorized Dealers pekee nchini Tanzania.
Muonekano wa ndani wa Banda letu la MeTL Group ukiwa umenakshiwa kwa mabango pamoja na TV za LG zinazoonyesha matangazo mbalimbali ya bidhaa zetu.
Mmoja wa wateja akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wetu waliobobea wa vipozi kwenye banda letu la MeTL Group.
Watu wanatakaje kupendeza.....!! bado wewe tu hujajipatia kitenge chako na Khanga....kwa bei nafuu kabisa katika msimu wa Sabasaba.
Baadhi ya ushers wanaotohuduma kwa wateja ndani ya banda la MeTL GROUP wakipozi kwenye Big Screen ya LG inayoonyesha tangazo la bidhaa mpya ya "MO BEAUTY SOAP" ambapo Balozi wake ni mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.
Mmoja wa kikundi cha uhamasishaji kwenye banda la MeTL Group akikata kiu yake na kinywa chenye ladha tamu kabisa ambacho kitaingia sokoni hivi karibuni "MO Portello" kinachouzwa ndani ya banda hilo.
Aaaah kinywaji safi kabisa...sasa nimekata kiu yangu...!! Unakaribishwa na wewe pia kukijaribu kinauzwa kwa bei nzuri kabisa ya offer katika msimu huu wa Sabasaba.
Mimi napenda "MO Portello" wewe je....??
AGRO MeTL wauzaji wa Mbolea na Matrekta ya kisasa ambayo ni imara na bora kwa mazingira yetu ya Tanzania yapo kwenye banda letu...Kilimo kwanza ndio mpango mzima...!!
Mambo ya Katani yanahusika pia ndani ya banda la MeTL Group kwenye viwanja vya Sabasaba.
Mambo ya Ugali, Maandazi na bidhaa mbalimbali za nafaka zinapatikana pia bila kusahau MO SEMBE..Unga safi kabisa wa kupikia.
Mambo ya usafi pia yanahusika jamani eeeeh...Sabuni za kufulia za unga zenye kuondoa madoa sugu na uchafu wa aina zote zinapatikana pia wewe tu na pochi lako.
Watoto wakipata maelezo kutoka kwa mhudumu wa vinywaji vya MeTL Group kwenye banda letu ndani ya maonyesho ya Sabasaba.
Watoto wakipata Ukodak baada ya kuyakubali maji safi ya kunywa kwa gharama nafuu kabisa yanayotengenezwa na MeTL Group.
Kata kiu yako kwa kujichagulia kinywaji ukipendacho hapa ndani ya banda la MeTL GROUP.
Mmoja wa wateja akiangalia tangazo la bidhaa mpya ya MO BEAUTY SOAP ambapo Balozi wa sabuni hiyo ni mrembo aliyewahi kushitaji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.
Mfanyakazi wa MeTL Group akitoa maelezo ya ubora wa maji safi ya kunywa yenye viwango vya kimataifa. Unakaribishwa sana kuuliza maswali mbalimbali ndani ya banda letu.
Kikundi cha NOMA SANA Group kikitoa burudani nje ya banda la MeTL Group kuwatumbuiza wakazi wa jiji wanaotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini.Kwa picha zaidi ingia hapa