AJALI YA MAPOROMOKO KILIMANJARO YAUA MMOJA
Jana majira ya saa kumi
alfajiri kumetokea ajali ya maporomoko ya mawe katika eneo la juu la
Mlima Kilimanjaro la Hans Meyer na kusababisha kifo kwa mwanafunzi Malata
Thomas kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli .
Aidha, mwanafunzi mwingine
Matenga S.J alivunjika mguu wake na anaendelea na matibabu katika hospitali
ya KCMC mjini Moshi.
Wanajeshi hawa walikuwa
pamoja na wenzao 265 walikuwa katika mafunzo yao ya kawaida ya ukakamavu
katika Mlima Kilimanjaro.
Shirika la Hifadhi za
Taifa linaendelea na taratibu za kufahamu chanzo cha kutokea kwa ajali
hiyo na taarifa kamili itatolewa kwa umma mara baada ya kukamilika.
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
15.07.2014