MEGATRADE YAIPIGA JEKI MOSHI VETERANI KWENDA KUKIPIGA TABORA SIKU KUUU YA NANE NANE.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Investiment Ltd ,Kanda ya Kaskazini, Edmund
Rutaraka,akikabidhi hundi ya kiasi cha shilingini milioni moja kwa mwenyekiti wa klabu ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro Tumaini Mungete .wengine ni baadhi ya viongozi wa klabu ya Moshi Veterani,Wilson Stephen na Aggrey Makia(upande wa kulia) upande wa kushoto ni wafanyakazi wa Megatrade mkoani Kilimanjaro.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Investiment Ltd ,Kanda ya Kaskazini, Edmund
Rutaraka,akikabidhi hundi ya kiasi cha shilingini milioni moja kwa mwenyekiti wa klabu ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro tumaini Mungete(kulia).
Hundi iliyotolewa na Megatrade kwa timu ya Moshi Veterani.


 TIMU ya soka ya Moshi Veterani ya mkoani Kilimanjaro iko katika
mazoezi makali kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Watumishi Veterani mchezo utakachezwa wakati wa sherehe za Nane nane zitakazofanyika mwezi ujao.
Wakati Mavetrani hao ambao wanajitamburisha kama “Wazee wa
Safari”wakiwa katika maandalizi hayo kampuni ya Megatrade ya jijini Arusha imenogesha maandalizi hayo baada ya kukabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni moja kwa uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya safari hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi,makao makuu ya timu hiyo ,Moshi Club ,Meneja Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Kanda ya Kaskazini, Edmund Rutaraka, alisema Megatrade pia imejikita katika kusaidia sekta ya michezo ikiwa ni sehemu ya kuboresha michezo nchini.
“Megatrade tunajua kwamba michezo ni furaha ,michezo ni uhai,sasa hawa wenzetu wa Moshi veteran wanenda kucheza Tabora,tumeona ni vyema tukawapa sapoti ikiwa ni sehemu ya kuboresha michezo nchini na mkoa wa
Kilimanjaro ,na hawa watakuwa mabalozi wtu wazuri wa kinywaji cha K-Vant,”alisema Rutaraka.
Aliyataka makampuni ,taaisisi na wadau wengine wa michezo mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza katika kusaidia wanamichezo pamoja na vilabu ili kuweza kusukuma gurudumu la michezo katika mkoa wa Kilimanjaro kwa kupata timu iliyobora zaidi katika mashindano na hata ligi kuu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Moshi Veteran, Tumaini Mogete, alisema maandalizi ya safari hiyo yanaendelea vizuri huku akitoa shukrani kwa uongozi wa kampuni ya Megatrade Investiment Ltd kwa kutoa mchango wao
katika kufanukisha safari hiyo.
"Maandalizi ya timu yetu yako vizuri ,zaidi niendelee kuwahamaisha wenzangu kufika mazoezini kwa ajili ya kuweka miili yao safi …….Tayari tumecheza michezo kadhaa kama sehemu ya mazoezi  kabla ya mechi iliyo mbele yetu na sasa tunatarajia kucheza mchezo wa mwisho na timu ya Arusha kabla ya safari"alisema Mungete. .



Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post