Picha
ikionyesha jinsi maj i yenye kemikali yanavyotiririshwa toka katika
kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge
akiangalia uharibifu wa mazingira uliosababishwa na maji yenye
kemikali yanayotiririshwa na kiwanda cha NIDA. Anayemfuatia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC Bonaventura Baya, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete.
Jengo la kiwanda cha NIDA likionekana kwa nje
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge
akiongea na Menejimenti ya kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA
Textiles kuhu kiwanda hicho kinavyoharibu mazingira kwa kutiririsha maji
yenye kemikali katika mto kibangu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith
Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake aliyoifanya
katika kiwanda cha NIDA textiles jijini Dar es Salaam
…………………………………………………
Rai imetolewa kwa wawekezaji wote
Nchini kuhakikisha wanajali na kutunza Mazingira.Hayo yamesemwa jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Binilith
Mahenge wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza
nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela katika kata ya Kigogo jijini
Dar es Saalam.
Kiwanda hicho ambacho
kinalalamikiwa na wananchi kuwa kinatiririsha maji machafu yenye
kemikali katika mto kibangu uliopo pembeni ya kiwanda hiko ambako
wananchi wanalima mbogamboga kando yamto huo na wanatumia kula pia
wanauza ili kujipatia kipato pasipo kujali athari zilizopo kwenye maji
hayo yenye kemikali.
Akiongea na Menejimenti ya kiwanda
hiko Dkt. Mahenge baada ya kutemebelea mto huo na kujionea maji
yalivyoathiriwa na kemikali zitokazo kiwandani, aliitaka Menejimenti ya
kiwanda hiko kuacha mara moja kutiririsha maji yenye kemikali katika mto
kibangu na hivyo basi kuchukua hatua za kitaalamu ili kuondoa kemikali
zilizopo kwenye maji hayo.
Akiongea kwa niaba ya Menejimenti
ya Kiwanda Afisa Utawala Mohammed Olewo aliahidi kwamba watafanyia kazi
maagizo ya Waziri kwa ufasaha na wanaahidi watarekebisha makosa yote
yaliyotokea pia watadumisha na kutunza mazingira.
Ziara hiyo ni moja ya ziara za
Waziri anazofanya kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam
kwa ajili ya kukagua utunzaji wa mazingira.