AZANIA BANK LTD YAFUTURISHA WATEJA WAKE NA YATIMA KITUO CHA MITINDO HOUSE FOUNDATION

 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Bwa.Singili alisema kuwa Benki ya Azania ni kama sehemu ya jamii, watajitahidi kutoa msaada kwa jamii katika Nyanja za elimu,afya na kusaidia yatima kila nafasi na uwezo unaporuhusu.Benki ya Azania pia iliwaalika Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa  benki ya Azania imekuwa sasa na kufikia matawi 15 ikilinganishwa na matawi matatu waliyokuwa  nayo mwaka 2007,alisema kwa Dar es salaam pekee wana jumla ya matawi 05. ''tunawashukuru wateja wetu,kwani bila uwepo wao tuingefika hapa,tunapenda kuwahakikishia kuwa tunaendelea na juhudi zetu za nia ya kutaka kuwa na teknolojia ilio sahihi'',alisema MKurugenzi huyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo pamoja na waalikwa wengine kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.
 Afisa mkuu maendeleo ya biashara kutoka benki ya Azania,Bwa.Othman Jibrea akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar Es Salaam.
 Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania sambamba na wadau wengine wa benki hiyo,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar Es Salaam.
Sheikh Abdulrahman Ali Issa akitoa shukurani za dhati (kwa niaba ya sheikh wa Mkoa Dar Es Salaam),kwa uongozi wa benki ya Azania kwa kutoa mwaliko wa futari kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo watoto yatima kutoka kituo cha Mitindo House Foundation..
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakipakua ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post