KITU KINACHOSADIKIWA KUWA NI BOMU KIMERUSHWA NA KUJERUHI WATU WAWILI KATIKA ENEO LA MAJENGO CHINI JIJINI HAPA
AKIONGELEA TUKIO HILO KAMANDA WA POLISI MKOANI HAPA SABASI ALISEMA KUWA TUKIO HILO LILITOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO WAKATI MAJERUHI HAO WAKIWA WANAKULA CHAKULA CHA USIKU KIJULIKANACHO KAMA DAKU
ALIWATAJA WATU AMBAO WAMEJERULIWA KUWA SUDI ALLY SUDI PAMOJA NA JEMSI MALLE
ALISEMA KUWA MAJERUHI WOTE WAMEJERULIWA VIBAYA KATIKA ENEO LA MIGUU
SABAS ALIBAINISHA KUWA MPAKA SASA AMNA MTU AMBAYE ANASHIKILIWA KWA TUKIO HILO NA JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUWASAKA WATUHUMIWA