Mamlaka ya Mapato nchini imeanzisha mfumo wa kutoa stempu kwa kazi za wasanii ili kudhibiti unyonywaji wa kazi hizo unaofanywa na baadhi ya wasambazaji na wazalishaji feki hivyo kuwafanya wasanii wanufaike na kazi zao pamoja na kulipa kodi kwa serikali.
Akizungumza
na Wasanii wa muziki na filamu jijini Arusha ,Afisa elimu kwa mlipakodi
TRA,Frank Mwaselela amesema kuwa mfumo huo tayari umerasimishwa
kisheria na baada ya kutoa elimu kwa wasambazaji na wasanii hakuna kazi
yeyote itakayoruhusiwa kuuzwa pasipo kuwa na stempu.
Afisa
huyo amesema kuwa mfumo huo utawasaidia wasanii kutoibiwa kazi zao na
pia kazi zao kuwa na ulinzio wa kisheria baada ya kupitia taratibu
sahihi ambazo ni kuzisajili baraza la sanaa (BASATA) Na pia kwa baraza
linalohusika na haki miliki (COSOTA).
Naye
Afisa Kodi Msafiri Mbibo kutoka makao makuu ya TRA amesema kuwa mfumo
huo wa stempu umeanza mwaka jana utasaidia kuondoa wimbi kubwa la
wizi na uharibifu wa kazi za sanaa .
“Mpango
huu utasaidia kuhakikisha kuwa wasanii kuwa mikataba inayozingatia
haki za wasanii,tayari tuimeshaanza kufanya operesheni kuwakamata
wanaouza kazi zisizo na stempu na kuharibu mashione mkoa wa Dar
tutaelekea mikoani pia” Alisema Afisa huyo
Katibu
wa Chama cha Wauzaji wa kazi za wasanii jijini hapa James Male amesema
kuwa jitahada zinazofanywa na TRA na Serikali ni nzuri na ameiomba
mamlaka hiyo kuzitazama kazi walizonunua miaka ya nyuma kabla ya
kuanzishwa kwa mfumo wa stempu.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wasanii mkoani Arusha ,Kassim Digega ameipongeza mamlaka
hiyo kwa kuonyesha nia ya dhati ya kulinda kazi zao ili waweze kunufaika
na kulinufaisha taifa kwa kulipa kodi.