JESHI LA POLISI MKONI ARUSHA YAANZA MSAKO MKALI WA KUYAKAMATA MAGARI YA KUSAFIRISHA ABIRIA YANAYODAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA KUSAFIRISHA ABIRIA




Baadhi ya magari yaliyokamatwa na jashi la polisi kikosi maalum cha usalama barabarani mkoani Arusha mara baada ya kugoma kusafirisha abiria kwenda Olasiti walikopangiwa na SUMATRA na badala ya yake kusafirisha abiria kwingineka
           

           Jeshi la polisi kikosi maalum cha usalama barabarani jijini Arusha imetangaza opereshen maalum ya kuyakamata ikiwemo kuyafutia leseni baadhi ya magari ya kusafurishia abiria yatakayobainika kukiuka taratibu za kusafirisha abiria
           Hayo yamebainishwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha kamanda Marison Mwakioma wakati akizungumza na woindeshizza blog ambapoamesema kuwa wamekuwa wakipokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi wakilalamikia baadhi ya magari ya kusafirishia abiria kutoka jijini Arusha kwenda maeneo mbalimbali  nje ya jiji kukiuka taatibu za kusafirisha abiria ikiwemo mengine kutoelekea walikopangiwa kusafirisha abiria huku mengine yakikatiza ruti na kupelekea abiria kutofika wanakoelekea kwa muda muafaka kwa sababu ya kucheleweshwa wakati wakitafutiwa gari lingine
             Mwakioma ameongeza kuwa kufuatia malalamiko hayo aliagiza  askari wa kitengo chake cha usalama barabarani kuanza kazi ya kuchunguza malalamiko hayo ambapo tayari wameshakamata baadhi ya magari yaliyokiuka taratibu za kusafurisha abiria kutoka jijini Arusha kwenda Olasiti na badala yake kuelekea kwingineko na kuwafanya wananchi wa Olasiti kupata adha ya usafiri  ambapo muda wowote wamiliki wa magari hayo wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka hayo yanayowakabili.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post