CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) jijini Arusha kimepata pigo baada ya
aliyewahi kuwa Diwani wake, Amos Mwanga kutimkia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA).
Mwanga alisema jana ameamua kujiunga na CHADEMA ili asaidie juhudi za
kupambana na mafisadi waliopo serikalini wanaomaliza rasilimali za
nchi kwa manufaa binafsi.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani hapa, Ephata Nanyaro alimkabidhi
Mwanga kadi ya CHADEMA yenye namba 229791 na kurejesha kadi ya CCM
namba 64141 iliyotolewa Juni 1988.
“CHADEMA imesaidia kupambana na ufisadi serikalini, nimeona niungane
nao ili niongeze nguvu ya mapambano… hatuwezi kukaa tukidanganyana kila
siku huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma muhimu,”
alisema Mwanga.
Baada ya kumkabidhi kadi hiyo, Nanyaro alimkaribisha Mwanga kwenye
uwanja wa mapambano ya kudai haki za wananchi huku akimwagia sifa kuwa
ni kiongozi mahiri.
Mwanga alikuwa diwani wa Levelos kuanzia 2005 hadi 2010 aliposhindwa na mgombea wa CHADEMA, Nanyaro kwenye uchaguzi mkuu
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia