Haris Fetahović, Daniel Bigas Alsina, Dino Julardžija
PRESS RELEASE
SABMiller
Dar es Salaam, Tanzania, July 31, 2014
Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 3:16 asubuhi
Makocha wa FC Barcelona wawasili kutoa mafunzo kwa makocha wa Tanzania
CASTLE
Lager, bia inayoongoza barani Afrika na FC Barcelona, moja kati ya timu
kubwa zaidi za soka duniani wameshirikiana kuleta makocha kutoka klabu
hiyo yenye makao yake huko Camp Nou, Hispania ili kutoa mafunzo ya mbinu
za soka kwa makocha wa Tanzania wiki hii. Makocha hao wa FC Barcelona
ambao wataendesha mafunzo hayo wamefika jijini Dar es salaam leo
(31/8/2014).
Mafunzo
hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kwa siku
mbili zijazo ambazo ni tarehe 1 na tarehe 2 Agosti na yataendeshwa na
makocha waliobobea kwenye mbinu mbalimbali za kandanda ikiwemo Tiki
Taka.
Makocha hawa ni Daniel Bigas Alsina and Isaac Oriol Guerrero Hernandez kutoka Shule ya Soka ya FB Barcelona.
Mafunzo
haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano uliosainiwa mwaka jana kati ya
FC Barcelona na Castle Lager ambayo ni bia rasmi ya FC Barcelona barani
Afrika. Vilevile, mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano huu
kwa jamii.
Kupitia
mafunzo haya, makocha 30 waliobahatika kutoka ligi kuu na ligi daraja
la kwanza watapata fursa maalum ya kujifunza mbinu mbalimbali za mazoezi
zinazotumiwa na FC Barcelona na kufanikiwa kuwatengeneza baadhi ya
wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi duniani.“Tuna
shauku kubwa sana kuona mafunzo haya yanakuja Tanzania na tunafurahia
kupata nafasi ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inatuunga mkono.
Tunaamini mafunzo haya yatawanufaisha makocha na wachezaji wa Tanzania
katika siku zijazo,” alisema Fimbo Buttallah, Meneja Masoko wa Kampuni
ya Bia Tanzania.
“Castle
Lager ina historia kubwa na soka barani Afrika na tukio hili litazidi
kuimarisha uhusiano uliopo kati ya bia namba moja Afrika na mchezo namba
moja kwa kupendwa barani Afrika.”
Mafunzo
haya kwa makocha yatahusisha mafunzo ya darasani kwa nadharia na
uwanjani kwa vitendo. Ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo, makocha hao
watatoa baadhi ya siri za mafanikio ya FC Barcelona ili kusaidia kuleta
utaalamu wa kimataifa kwenye soka la Tanzania.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia