Wafanyakazi wa Benki ya Twiga
Bancorp wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda lao mapema leo ,kwenye
maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es
Salaam.
Mama Mjasiliamali wa kampuni ya Tree
of
Life,Bi.Jessica Msamba akifafanua jambo kwa Afisa Masoko wa Twiga
Bancorp,Bwa.Adalbert Alchard mapema leo mchana kwenye maonesho ya
38 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam.Bi Jesca ni mmoja wa
wateja wakubwa wa benki hiyo na amekuwa
akiendesha biashara zake za ujasiliamali kupitia mikopo mblimbali ya benki
ya
Twiga Bancorp.
Mkuu wa
Shughuli za Kibenki
wa Twiga Bancorp,Bwa.Richard Kombole akielezea jambo kwa baadhi ya
Wanahabari
hawapo pichani,mapema leo kwenye maonesho ya 38 ya biashara ya
kimataifa
jijini Dar es Salaam,waliotaka kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo
na
benki hiyo kwa wateja wao,kulia ni Meneja wa Tawi wa benki hiyo Makao Makuu
jijini Dar,Bwa.Sigisbert Komba na nyuma
ni Msimamizi wa Usalama wa Majengo benki ya Twiga
Bancorp.
Afisa
Masoko wa Twiga
Bancorp,Bwa.Adalbert Alchard akihojiwa na moja ya chombo cha habari,mapema
leo mchana kwenye maonesho ya
38 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam,kuhusiana na huduma
wazitoaza kwa wateja wao,Bwa.Adalbert amesema kuwa benki yao,Twiga Bancorp
inatoa huduma mbalimbali kama vile Akaunti ya Akiba,Akaunti ya
Biashara,Akaunti ya Amana,Huduma za Kibenki za Kimataifa,mikopo,utumiaji wa
fedha na nje ya nchi,''Dira yetu kubwa ni kuwa taasisi ya kifedha
inayoongoza kutoa huduma bora za kibenki nchini'',alisema
Bwa.Adalbert.
Baadhi ya Wateja walipatiwa
vipeperushi vilivyosheheni huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo ya
Twiga Bancorp.