Taka zilizokutwa na kamera yetu ya libeneke la kaskazini blog zikiwa zimezagaa hadi katika lango kuu la kuingilia kwenye soko hili la samunge
Ni maji taka yaliyochanganyika na kinyesi
yanayodaiwa kutiririka kutoka kwenye vyoo vya soko la NMC maarufu kama
soko la SAMUNGE kutokana na vyoo hivyo kujaa na kuelekea kwenye maeneo
ambapo wafanyabiashara wanamofanyia biasha
Baadhi ya watu wengine wanadaiwa kunufaika kutokana na uchafu huo ambao wafanyabiashara wanaeleza kuwa kero kwao
Wakazi katika Soko la NMC maarufu ka Soko la SAMUNGE wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kutokana na hali mazingira ya soko hilo yalivyo hivi sasa ambapo Uongozi wa jiji la arusha umetakiwa kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo hilo
Kwa mujibu wa wafanyabiashara waliozungumza na libeneke la kaskazini blog wameeleza kuwa mbali na uchafu kuzagaa hadi wanapofanyia biashara zao kutokana na kutobebwa kwa wakati,hivi sasa wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kutokana na vyoo wanavyovitumia kujaa na kupelekea maji taka yaliyochanganyika na kinyesi kuanza kutiririka hadi kwenye maeneo wanakofanyia biashara
kufuati malalamiko libeneke la kaskazini blog ilimtafuta afisa afya wa jiji la Arusha ndugu Jemsi Lobikoki ambae alikiri kuwepo kwa tatizo hilo ila akdai kuwa hivi sasa wapo njiani kulitataua chemba za choo hicho cha soko la Samunge zimekuwa zikiziba kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kutupa taka ngumu kwenye shimo la choo hicho
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia