mwanamuziki maarufu wa reggae barani afrika jhikomani apa akiwa anapiga jitaa
Mwanamuziki maarufu wa Reggae
barani Afrika Jhikoman ambaye yupo katika ziara ya kikazi barani
ulaya,juzi alitua katika mji wa Tubingen,Ujerumani kwa ajili ya
kushiriki katika maonyeso makubwa 5th International African Festival
Tubingen 2014,
ambako amealikwa na shirika
la Afrikaktiv Org. Jhikoman amelamba deal la mkataba wa kudumu wa
kutumbuiza katika onyesho hilo,pia amepata nafasi za kualikwa na
kutembelea miradi mbali mbali ya utamaduni nchini ujerumani zikiwemo
shule na tahasisi za muziki,ambazo amekuwa kivutio kikubwa na tahasisi
hizo zimehaidi
kwenda Bagamoyo kwa kupata ujuzi zaidi wa kimuziki na utamaduni .