Bendi
Mahiri na Machachari Jijini Dar Skylight Band wametoa wimbo wao wa
Tano ikiwa ni muendelezo wa kutoa nyimbo tofauti tofauti kupitia Studio
yao ya kisasa ya Skylight Production.
Akiongea
na Mtandao huu Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba AK47 amesema wimbo huo
unaitwa “Pasua Twende” ambo umetungwa na Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo
Dk. Sebastian Ndege akishirikiana na wanamuziki wa Bendi hiyo.
Aneth
akaongezea kwamba wimbo huo ni wa tano kutolewa katika mtiririko wa
nyimbo zao zilizokwisha kutoka na imetengenezwa ndani ya studio yao ya
Skylight Production chini ya Produzya Joobanjo.
Isikilize hapa chini na Ijumaa hii utapa fursa ya kusikiliza ikipigwa LIVE ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.