Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya  siku tatu  katika jiji la Arusha .
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Stanslaus MuIongo Wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Mulongo alisema kuwa ziara hiyo inaanza  rasmi  november moja ambapo ataanza rasmi kuzindua  hospitali ya Oluturmet iliyopo katika halmashauri ya arusha vijijini ambapo hapo awali ilikuwa ni kituo cha afya ambapo kwa sasa imepandishwa hadhi .
Aidha alifafanua kuwa siku hiyo hiyio  ya kwanza ataweka jiwe la msingi katika barabara zinazojengwa jijini hapa ambazo mradi huo ni kwa hisani ya  benki ya dunia pamoja na serikali yaTanzania  baada ya hapo alisema kuwa mheshimiwa rais atamalizia na uzinduzi wa nembo ya jiji la Arusha ambapo itazinduliwa rasmi katika makumbusho ya jiji ambapo itaambatana na sherehe za uzinduzi huo ambapo rais atatumia fursa hiyo kuongea na wananchi wa jiji la Arusha katika uwanja wa kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid.
November mbili Rais ataendelea na ziara yake katika taasisi ya Nalson Mandela ambapo atazindua rasmi taasisi hiyo  na baada ya hapo atatembelea kiwanda cha kutengenezea vyandarua  cha A to Z ambapo ataona shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho pamoja na kusikiliza changamoto zinazoikabili na kuona namna ambavyo serikali itaweza kuwasaidia kutatua changamoto hizo.
Mulongo alisema kuwa siku ya tatu Rais anatarajia kwenda kufungua shule ya msingi ya Sokoine iliyopo ndani ya eneo la jeshi  la kulinda  taifa(JWTZ)  iliyopo wilayani Monduli  na baada ya hapo ataenda kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara kutoka Arusha hadi minjingu.
Mulongo alitoa wito kwa wananchi wa jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo wa jiji la arusha hususan pale ambapo Rais atakapo hutubia wananchi wa jiji la Arusha katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid .

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo alibainisha kwamba kupatikana kwa cheti hicho kunaipa mamlaka iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha kutumia rasmi hadi ya Jiji.

“Hii intaufanya kubadilisha kuanzia nyaraka zote za vitendea kazi pamoja na Nembo ya Manispaa ambapo sasa tutatumia Nembo mpya.
Alisema Halmashauri hiyo ilianza tangu mwaka 1948 ikiwa ni Halmashauri ya Mji baada ya kukua kwa mji  ambapo ilibandishwa hadi na kuwa Manispaa mwaka 1980.

Kutokana na kupanuka kwa shughuli katika eneo la kilomita za mraba 93, Serikali iliamua kupandisha hadhi ya eneo hilo hadi kufikia kilomita za mraba 2,008.

 “Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Serikali namba 341 la Oktoba 14, mwaka 2011,” alisema Meya Lyimo.