BREAKING NEWS

Tuesday, October 30, 2012

WASANII WA MKOA WA ARUSHA WAMVAA MEYA

meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo akiwa anaongea na wasanii ambao walimfata kulalamikia kutoshirikishwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa jijini arusha ikiwemo pamoja na kutopewa kipaumbele katika sikukuu za uzinduzi wa nendo wa jiji la arusha
 wasanii wa muziki na vikundi mbalimbali vya maigizo mkoani Arusha wamewataka  viongozi wa serikali kutowadharau na kuwashirikisha kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo jijini Arusha.
hali hiyo imetokea wakati zikiwa zimebaki siku chache ili kufanyika uzinduzi rasmi wa Jiji la Arusha baada ya wasanii hao kudai kutoshirikisha kwa lolote.
akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake msanii wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari alisema kuwa wameshangaa sana kusikia kuwa msanii kutoka dar es salaam Diamond Platnum atakuja kutumbuiza  ilihali wao wapo na hawana taarifa yeyote.
nakaaya alisema kuwa hawana tatizo na Nasibu Abdul(Diamond) ila walichokiona ni dharau kutoka kwa afisa Utamaduni wa manispaa kwa kutoonyesha ushirikiano na  badala yake wamepewa taarifa ya kufanya kitu jana usiku baada ya wao kuulizia.
"Tumeshanga sana hii ni dharau wasanii wa arusha hatuheshimiki kabisa na tumeuliza ndo tunaambiwa eti tuandae kitu kwa ajili ya uzinduzi dah yani inakatisha tamaa sana alafu afisa utamaduni mwenyewe anatuona anatupotezea"alisema nakaaya
Aidha nakaaya alimpongeza Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Gaudience Lyimo kwa kutoa ushirikiano wake kwao na kuahidi kushirikiana nao kwa madai ya kilichofanyika ni makosa ya kibinadamu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wasanii mkoa wa arusha Hussein Sechonge alikemea vikali tabia hiyo kwa kuwa wasanii wana mchango mkubwa wa kufikisha ujumbe na kuwataka viongozi kuwa wazalendo.
aidha walimtaka afisa utamadumi manispaa  Juma Sule kutoa ushirikiano kwa wasanii wa hapa kwa kuwab wao ndio wanajua kila kitu kuhusu manispaa na sio Diamond..
''tunamshangaa sana hapa kuna wasanii 70 sasa nashangaa kwenye mwenge aliletwa Juma Nature wakati wao wapo hapa na hawafahaamu kitu chochote sio vizuri"alisema Sechonge
hadi mwandishi wa libeneke la kaskazini anaondoka katika ofisi za manispaa ya arusha wasanii hao walikuwa  nje ya ofisi ya meya wakisubiri kujadiliana namna ya kufanya na kumaliza tofauti hiyo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates