BREAKING NEWS

Thursday, October 25, 2012

TUKIO LA UTATA LAGUBIKA ARUSHA,KATIBU WA BAKWATA ALIPULIWA BOMU NYUMBANI KWAKE


 TUKIO la Utata lililomtokea Katibu  wa Baraza la Waislam (BAKWATA)  Mkoa wa  Arusha. Shekhe Abdulkarim Jonjo la kulipuliwa na kitu kinachosadikiwa  kuwa ni bomu nyumbani kwake limezua maswali ya kujiuliza miongoni mwa viongozi pamoja na majirani wa eneo analoishi kiongozi huyo lililopo Esso.

Tukio hilo lilogubikwa na utata  limetokea juzi saa 6:30 usiku eneo  Sokoni One lililopo  Esso ,Jijini Arusha baada ya majeruhi ambaye ni Shekhe Jonjo kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu ambalo lililipuka usiku eneo la chumbani kwake na kuacha shimo kubwa kwa nje.

Akisimulia tukio hilo katika Hospitali ya Mount Meru iliyopo Jijini Arusha, katika wadi wa majeruhi, Jonjo alisema alifika nyumbani kwake juzi saa 1:00 usiku umeme ulikuwa umekatika na kuingia ndani kwake kisha alipitiwa na usingizi lakini ilipotimu saa 4:00 usiku umeme ulirudi ndipo aliposhtuka na kuamka kuchaji simu yake ya kiganjani.

Baada ya kuacha simu hiyo ikiingia chaji aliendelea na usingizi na ilipotimu saa 6:00 usiku hadi saa 6:30 usiku ghafla aliona kitu kinawaka chumbani kwake aliposhtuka na kujiuliza ni kitu alikwenda kukishika na mkono ndipo kitu hicho kilipomlipukia na kumpa majeraha sehemu za usoni ,machoni ,mkononi na kifuani.

Alisema baada ya mlipuko huo alitopeza fahamu kwa muda na alipozinduka kwasbabu alikuwa peke yake familia yake ilikwenda Mkoani Tabora kwasababu ya msiba ,alipata akili ya kwenda kufungua mlango na kuwaomba msaada majirani wenake ambao walimuwahisha hospitali kupata matibabu zaidi.

"Nilikuwa peke yangu usingizini na niliposhtuka niliona kitu kinawaka kama vile utambi nikajiuliza ni kitu gani ndipo nilipopata akili ya kwenda kukishika na kikanilipukia sehemu mbalimbali za mwili,ukweli nimepoteza danu nyingi ,ila naskia maumivu".

Aidha  Mganga  Mfawidhi wa Hospitali ya Mount Meru ,Dk Ijosia Mlai  alisema walimpokea Katibu huyo juzi usiku akiwa katika hali ya maumivu na alipowasili hospitalini hapo alikuwa na kumbukumbu zake  ila amepata maumivu katika shemu mbalimbali za mwili ingawa si makubwa sana na hajavunjika sehemu yoyote.

"Tunaendelea kumpat huduma za matibabu lakini hajapata majeraha makubwa ni ya kawaida ila ameumia shemu a usoni,kifuani pamoja na baadhi ya shemu za mwili lakini majeraha ni yakawaida na si mkubwa".

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alifika Hospitalini hapo kumjulia hali na kumpa pole  kisha kwenda nyumbani kwa Katibu huyo na kuwasihi watu wa Arusha kuacha kuingiza tukio hilo la bomu na masuala ya dini kwani ni mapema mno kutoa majibu wakati kunatimu imeundwa ya Polisi, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwakushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama hivyo wataalam hao wa mambo ya milipoko kutoka JWTZ pamoja na tume hiyo watakapomaliza kuchunguza majibu yao ndiyo yatatoa tawira ya tukio hilo lililoghubikwa na utata.

"Tukio hili ni la utata kwani kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa wataalam hawa wa JWTZ na Polisi wanadai mlipuko wa bomu hilo umetokea ndani ya chumba cha Jonjo na si nje hivyo nimapema mno kusema ni bomu la aina gani au nani kafanya hivvyo tusibiri uchunguzi wa tukio hili ambalo nasema ni la utata".

Alisema wanataka kuchunguza jambo hilo kwa ukamini zaidi sababu ni la utata hivyo nawasihi wananchi wa Arusha kaucha kuingiza suala hili na masuala ya dini ,wacheni uchunguzi ufanyike maana mazingira  ya tukio hili kwa mujibu wa wataalam hawa  ni ya utata.

Naye mmoja wa wataalam kutoka JWTZ ambaye hakutaka jina lake litajwe , alisema mlipuko unavyotokea kama ingekuwa ni kwa nje lazima moshi ungekuwepo kwa nje lakini mlipuko huo umetokea kwa ndani ndio maana chumbani kwa Jonjo kumekutwa na moshi pamoja na nyufa za kuweka alama hivyo kwakitaalam mlipuko huo umeanzia ndani na kutokea nje.

"Hili tukio limeanzia ndani chumbani kwa Jonjo na si nje ya nyumba anayoishi ,hivyo siwezi kusema kwa undani lakini tunachunguza jambo hili tukimaliza taarifa kamili mtaipata kwa wahusika ,lakini kama mlipuko huu ungetokea nje lazima shimo lingekuwa dogo nje halafu kwa ndani likawa kubwa lakini hili tukio la utata kwani kwajinsi tunavyoona mlipuko huu umeanzia ndani ndani kunashimo dogo  na nje ya dirisha lake katika chumba anacholala kunaonekana shimo kubwa".

Nao majirani wanaoishi karibu na nyumba anayoishi Shekhe huyo, Mama Husna alisema majira ya saa 6:30 usiku waliskia mtikisiko mkubwa kwenye nyumba yao wakahisi ni majambazi na wakati wanapigiana simu ndipo walipogundua kuwa nyumba anayoishi Jonjo ndio pametokea mlipuko huo inagwa haawajui bomu hilo ni la aina gani.

Mpangaji anayeishi na Jonjo ,  Hillary Musa alisema aliskia mtikisiko katika nyumba wanayoishi yeye na waoangaji wenzake akiwemo shekhe huyo na alipotoka nje alidhani ni shoti ya umeme lakini ghafla alimuona Jonjo akihitaji msaada  ndipo walipomuuliza kulikoni naye alipowaeleza ilibidi waombe msaada kwa majirani na kumkimbiza Hospitalini hapo.


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates