BREAKING NEWS

Tuesday, October 30, 2012

FAINALI ZA REDD'S MISS TANZANIA KUFANYIKA TAREHE 03, NOVEMBER 2012 UKUMBI WA HOTEL YA BLUE PEAL (UBUNGO PLAZA)



Mkurugenzi wa Kampuni Lino Agency inayoandaa na kuratibu mashindano ya Miss Tanzania Bw. Hashimu Lundenga akizungumza hatua ya kukamilika kwa mashindano ya Urembo ya Kanda na kutangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang’anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya Jumanne tarehe 2 Oktoba 2012.
 
Mashindano ya Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo jumla ya 30 .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya Juu.

Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.

Baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.

Tunapenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza).


Kwa Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates