Meneja Mawasiliano wa shirika la
Tanesco Bi.Badra Masoud akiongea na waandishi wa habari juu ya mkutano
wa Mawaziri wa Nishati wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati mwa Afrika
unaotarajiwa kuanza jijini Arusha ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji
wa mkutano huo
Tanzania imebahatika kuwa
mwenyeji wa mkutano(5) wa mawaziri wanaosimamia Nishati ya Umeme kutoka
nchi 11 zilizo Mashariki na Kati mwa Afrika wanaounda mtandao wa
nishati na umeme maarufu kama”East Afrika Power Pool (EAPP) unaotarajiwa
kuanza rasmi kesho jijini Arusha
Hayo yamesemwa na Afisa
uhusiano wa shirika la umeme (TANESCO) Badra Masoud wakati
akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano huo mkubwa ambao
unatarajiwa kufanyika jijini hapa
Masoud alisema kuwa Tanzania
ni mwanachama wa mtandao wa (EAPP) ulionzishwa miaka 6 iliyopita ikiwa
na lengo la kurahisisha upitakanaji wa nishati ya uhakika ya umeme kwa
nchi wanachama wa EAPP kwa kujenga njia kuu ya kusafirishia umeme
unaounganisha nchi hizi.
Alifafanua kuwa Tanzania
inahitaji kuboresha maisha ya wananchi wake katika Nyanja nyingi kama
vile matibabu,elimu,upatikanaji wa maji safi na
salama,uzalishaji,Ongezeka la viwanda na kurahisisha matumizi ya
majumbani.
Alisema kuwa haya yote
yatawezekana tu kama kutakuwa na umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu
ili wananchi waweze kumudu gharama hizo bila matatizo yeyote.
Masoud alisema ili kupata
umeme wa uhakika na gharama nafuu,Mawaziri wa nchi hizi 11 watatoka na
mwongozo wa utekelezaji wa kuunganisha miundombinu ya njia kuu ya
kusafirisha umeme kwenye nchi za Afrika Mashariki na Kati mwa Afrika.
“kwa sasa tunanunua umeme bei
ghali sana kutoka kwa wazalishaji binafsi (Independent Power
Producer-IPP) ambao wanatuuzia umeme kwa bei ghali sana hivyo TANESCO
inaponunua umeme kwa bei ghali sana na kuiuza kwa bei kawaida
inaipelekea kupata hasara na hata kupandisha bei ili kukidhi gharama za
uendeshaji.”alisema Badra
Hata hivyo alisema kuwa mkutano
huo utatanguliwa na Wakurugenzi wa mashirika yaliyo na dhamana ya
kuzalisha,kusafirisha na kusambaza umeme,wakiwepo wadau wa Mamlaka za
Udhibiti wa Nishati ya Umeme wataanza mkutano wa awali utakaofuatiwa na
mkutano wa Mawaziri siku ya Jumamosi.
Alisema kuwa nchi wanachama wa
EAPP,ni Tanzania
,Kenya,Uganda,Ethiopia,Rwanda,Burundi,Libya,Egypt,Republic of
Sudan,Demokratic Republic of Congo(DRC) na Djbouti.