UCHAGUZI mdogo wa udiwani katika kata ya Darajambili Mkoani Arusha jana
umeingia dosari baada ya risasi kurindima hewani mfulululizo asubuhi ya
leo karibu na maeneo ya kupigia kura hali iliyozua taharuki kwa wakazi
wa kata hiyo waliokuwa wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura.
Risasi
hizo zinadaiwa kupigwa na mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua
Nassari
pamoja na mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM(Uvccm) wilayani
Arusha,Godfrey Mwalusamba mara baada ya kuibuka tafrani baina ya wafuasi
wa CCM na Chadema katika eneo la
Shule ya sekondari ya Felix Mrema.
Katika vurugu hizo dereva wa
aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Haleluya Natai pamoja na wafuasi wa
Chadema zaidi ya 15 walikamatwa na jeshi la polisi huku Nasari na
aliyekua
mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema wakitokomea kusikojulikana
lakini kisha baadaye walionekana katika viunga vya kupigia kura.
Hatahivyo,katika
hali isiyo ya kawaida naye mgombea wa Chadema katika kata hiyo,Prosper
Msofe alionekana akirandaranda katika vituo vya kupigia kura huku akiwa
na silaha yake aina ya bastola kiunoni hali ambayo ilizua mshangao kwa
wapiga kura wa kata hiyo.
Katika vurugu hizo inadaiwa kuwa Nasari
aliyekuwa akiongozana na lema wakiwa katika gari mojawapo walivamia
ngome ya CCM iliyopo karibu na ofisi za chama hicho kata ya daraja mbili
hali ambayo ilipelekea wafuasi wa CCM kuwavamia lakini Nasari alijiami
na kisha kufyatua risasi tatu hewani.
Hatahivyo,kada wa CCM
,Kabwelwa Mturuka alijeruhiwa mkononi kwa kukatwa na panga na watu
wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema wakati wa majibishano karibu na
kituo cha kupigia kura.
Katika vurugu hizo mwenyekiti wa UVCCM
wilaya ya Arusha Martin
Munis naye aliporwa simu yake ya mkononi na fedha ambapo alitoa
taarifa katika jeshi la polisi na kupewa AR/RB/13624/2012 ya shambulio
la kudhuru mwili dhidi ya Nasari na Lema.
Wakati huohuo,wafuasi
wa Chadema waliokuwa mita chache karibu na kituo cha kupigia kura cha
sekondari ya Felix Mrema baada ya zoezi la uchaguzi kwisha, wakati
wakisubiri matokeo, walivamia ofisi za CCM zilizokuwa karibu na kituo
hicho na kisha kujaribu kung”oa bendera ya chama hicho lakini jitihada
hizo zilizimwa na wafuasi wa CCM baada ya kumshusha kabla hajaikaribia
bendera hiyo.
Kwa upande wake,Nasari alipoulizwa juu ya hatua
yake ya kurusha risasi hewani alipinga vikali lakini alipotafutwa
Mwalusamba alikiri kurusha risasi hizo hewani huku akidai kwamba
alifyatua kwa lengo la kujihami.
Aidha saa nne usiku matokeo
yamekemilika na kutangazwa na Modest Lupogo kwa niaba ya kaimu
mkurugenzi wa jiji la Arusha Omary Mkombole ambapo alisema kuwa
idadi ya watu walioandikishwa kupiga kura ni 16295 lakini waliojitokeza
kupiga kura ni 3770 tu.
Akitangaza diwani mpya wa kata ya daraja
mbili Lupogo alisema kuwa Prosper Msofe aliibuka kidedea kwa kura 2193
kupitia Chadema, akifuatiwa na mpinzani wake Philip Mushi Philip
kupitia CCM aliyepata kura 1324, huku CUF ikipata kura 162, TLP wakipata
kura 42, na NSSR kuambulia kura 22
Kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Arusha,Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya matukio hayo alisema
kuwa jeshi la polisi wanawashikilia watu saba kwa tuhuma za shambulio
lamwili la aibu pamoja na la kuzuru mwili.
Alisema kuwa watu hawa
wanahusika na kumkamata mama mmoja ambaye jina lake halijafahamika na
kumpekua pekua sehemu za mwili wake wakidhani kuwa amebeba fedha za
kuwapa wapiga kura.
"sasa wakati wanampekuwa ndipo kijana mmoja
ambaye alijulikana kwa jina la Hamidu Mussa(32)aliamua kumpa msaada yule
mama sasa wakati anampa msaada ndipo
wakamkata na panga mkononi wakati huo huo ndugu Godfrey mwalusamba
alikuwa karibu na tukio hilo ndipo akamua kusogea ili kumsaidia mama
huyu na kijana huyu ndipo alipoamua kupiga risasi moja juu na vijana
wale wakatawanyika lakini jeshi la polisi lilifatilia na kuwakamata hawa
vijana saba"alisema Sabas
katika watu hao saba kamanda sabas
alimtaja mmoja wao jina kuwa ni Ringo Andwea (mungure) mkazi wa
daraja mbili pamoja na wenzake sita ambapo alisema wapo chini ya ulinzi
na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika.
Wakati
huo huo katika kata ya Bangata iliyoko wilayani Arumeru mkoani Arusha
akitangaza matokeo hayo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha
Halipha Idda alisema kuwa Olais Peter kupitia CCM ameibuka kidedea kwa
kura 1177 na kuwaacha wapinzani wake Erick Samson Mollel kupitia Chadema
kwa kura 881 huku Samweli Saimon Ndosi kupiti TLP akiambulia kura 3
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia