Jeshi la polisi Mkoni hapa
wakishirikiana na askari wa Hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro
(KINAPA)wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Long”ida Silayo (42)akiwa na silaha aina ya bunduki kinyume cha
sheria
Kamanda wa Polisi Lebaratus Sabas akiwa anawaonyesha wanahabari silaha aina ya bunduki aliyokutwa nayo mtuhumiwa
Akidhibitisha kukamatwa kwa
mtu huyo Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas
alisema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 13 oktoba majira ya 12:30
asubuhi katika kitongoji cha Nakilongosi katika kijiji cha Kamwanga
Wilayani Longido
Alisema kuwa Mafanikio hayo
yalipatikana baada ya askari hao waliokuwa doria kupokea taarifa kutoka
kwa raia wema kwakuwepo kwa mtu amabye anajishughulisha na uwindaji
haramu katika hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro akiwa na silaha kinyume
cha sheria kwa matumizi ya kuulia wanyama aina ya Tembo
“Kufuatia taarifa hiyo ndipo
askari wa jeshi la polisi na askari wa hifadhi ya taifa walikwenda
kufanya upekuzi katika nyumba tatu zinazomilikiwa na mtuhumiwa
huyo”alisema Sabas
Alitaja aina ya silaha aliyokutwa nayo mtuhumiwa huyo kuwa ni bunduki aina ya rifle yenye namba 2758J
Kamanda Sabas aliongeza kuwa
mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi mkali ambapo alihojiwa na askari
kuhusiana na uhalali wa silaha hiyo huku yeye mwenyewe akikiri kumiliki
isivyo halali
Hata hivyo mtuhumiwa huyo
anadaiwa kufanya uwindaji haramu hapa Nchini pamoja na Nchi ya jirani
Kenya huku akikiri kutumia silaha hiyo katika matukio ya ujambazi katika
maeno mbalimbali ya hapa na Kenya
Aidha kamanda Sabas alisema
kuwa wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi na baada
ya upelelezi wa awali kukamilika atafikishwa mahakamani
Mhifadhi Mkuu ya taifa ya Kilimanjaro (KINAPA)Erastus Lufungulo akiwa anaongea na wanahabari
Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu
ya taifa ya Kilimanjaro (KINAPA)BErastus Lufungulo aliwaambia
waandishi wa habari jijini hapa kuwa ujangili bado ni changamoto kubwa
kwao kwa kuwa ni mtandao ulioenea ndani ya jumuhiya ya afrika mashariki
Alisema kuwa mbali na mbinu
wanazotumia kuwa dhibiti wawindaji haramu hapa Nchini njia moja wapo ni
pamoja na kuwashirikisha wananchi kuhusu hao wawindaji haramu huku
akisema kuwa wananchi wasisite kushirikiana nao kwa kuwaibuwa majangili
hao kwa kuwa jamii inamchango mkubwa