Mbunge
wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (pichani), ametoa siku 14 kwa
magazeti mawili yatolewalo kila siku nchini kumsafisha kwa uzito
waliotolea habari ya kumhusisha kufyatua risasi kwenye kata ya Daraja
Mbili wakati wa uchaguzi mdogo, vinginevyo atayashitaki Baraza la
Habari Tanzania (MCT).
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini hapa jana, alisema ameshangazwa kuona
propaganda chafu dhidi yake zikiendeshwa kwa wazi na chuki kubwa. “Mimi
nilipita eneo la kupigia kura saa mbili kamili asubuhi nikaend kata ya
ya Bang’ata wilayani Arumeru nikiwa kama wakala mkuu, kusimamia
uchaguzi na tukio hili la kufyatua risasi limetokea mchana saa saba,
nashangaa naandikwa mimi,” alisema.
Alisema
kuwa kikubwa anachokiona ni kumpaka matope kupitia magazeti hayo.
Nassari alisema kuwa anachofahami fika magazeti hayo kupitia waandishi
hao wanatumiw ana watu kumchafua kwa sababu wanazojua wao, kufuatia
kushinda uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki. “Kwa kweli sasa
sitakubaliana kamwe na tabia hii, maana nachafuliwa kwa makusudi na
kusababisha wapiga kura wangu wajenge chuki dhidi yangu, alisema.
Kamanada
wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabasi, alipoulizwa alisema: “Mimi
silijui suala hili, nimesikia katika vyombo vya habari, ninachojua mimi
risasi zilifyatuliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Wilaya ya Arusha
(NEC), Godfrey Mwalusamba wakati akimwokoa Mussa Hamisi, aliyekatwa
panga, wakati akimwokoa mama mmoja aliyedaiwa kugawa pesa za kuhonga,
wapiga kura wa Daraja Mbili ili kuipigia CCM,”alisema.
Alisema
Mwalusamba alilazimika kufyatua risasi baada ya kumwona Mussa Hamisi,
akikatwa panga na kundi la watu hao walitawanyika na kuwa watu wanane
walitiwa mbaroni.
Chanzo gazeti la nipashe