Mtaalam wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro akitaja baadhi ya vikwazo vinavyo kwamisha uboreshaji wa Mazingira katika maeneo ya makazi ikiwemo uhaba wa maji na kutaka vikwazo hivyo viangaliwe upya na kuboreshwa sambamba na kutolewa kwa elimu ya Mazingira na uhamasishaji katika ngazi zote.
Amefafanua kuwa hata katika utekelezaji wa sera za serikali kama vile Kilimo Kwanza elimu ya matumizi sahihi ya Ardhi inapaswa kutolewa kwa wakulima ili utekelezaji wa sera hizo uwe na tija na ufanisi zaidi kwa manufaa ya taifa.
Afisa Misitu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Freddy Manyika akitoa nasaha zake kwa kusema kuwa sisi wananchi ndio tunatakiwa kuwa wa kwanza kufanya mabadiliko na sio kuilaumu serikali kwani ndio tunaozungukwa na mazingira.
Aidha pia ametumia nafasi hiyo kutangaza kuwa suala la mabadiliko ya hali ya hewa sio jambo la mzaha hivyo serikali inatakiwa kuwa na sera madhubuti zitakazo wawezesha wananchi kukabiliana na madhara yatokanayo na janga hilo ili kujitahidi kuirejesha ardhi na mazingira yetu kwa ujumla katika hali bora.
Mtaalamu wa Ikolojia Profesa Raphael Mwaliosi akitoa mada wakati wa majadiliano ya hadhara yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja huo ambapo amechambua changamoto baina ya Mazingira na Mabadiliko ya hali ya Hewa hapa nchini na jitihada za kukabiliana nazo.
Ameongeza kuwa changamoto zaidi zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa zinaleta athari mpaka katika Nyanja ya kiuchumi akitolea mfano sekta za Kilimo, Maji, Nishati, Afya, Misitu, Uvuvi na Utalii.
Pichani Juu na Chini Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini wakitoa maoni yao katika mjadala wa wazi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee ambapo wamelalamikia baadhi ya Sera za Serikali zisizotekelezeka wakatu wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa kusheherekea miaka 67.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali jijini waliohudhuria Mjadala wa wazi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa katika kusheherekea miaka 67 tangu kuanzishwa.